November 15, 2024

Dkt. Yonazi Awataka Wakandarasi Kukamilisha Ujenzi Majengo Ya Mji wa Serikali Kwa Wakati Na Ubora

0

Na Valentine Oforo Dodoma 
 
KATIBU
Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu ( Sera, Bunge na Uratibu) Dkt. Jim Yonazi
amewataka wakandarasi kuzingatia ubora katika ujenzi wa majengo ya Ofisi
za Serikali katika eneo la Mtumba na kukamilisha kwa wakati.
 

 

 

 
Ametoa
kauli hiyo alipokagua maendeleo ya ujenzi wa majengo ya Ofisi za
Serikali unaoendelea eneo la Mtumba Jijini Dodoma  ambapo amekagua
baadhi ya majengo ikiwemo la Ofisi yake, Ofisi ya Rais Menejimenti ya
Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali,
Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Wizara
ya Maji na Wizara ya Fedha.
 
Dkt.
Yonazi amehizima kwa kila mkandarasi kuhakikisha anazingatia ubora na
viwango vinavyotakiwa huku wakizingatia thamani ya fedha zilizotolewa na
Serikali.
 
 

 

 

 
“Dhamira ya
Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni kuona majengo haya
yanakamilika kwa wakati na yawe na viwango vinavyotakiwa, bila kuwa na
delays zozote ili kuhakikisha watumishi wote wanahamia haraka na
kuendelea na utekelezaji wa majukumu yao na kuliletea Taifa maendeleo
yanayotakiwa,” alisema Dkt. Yonazi.
 

 

 

 
Awali
alipongeza kwa hatua iliyofikiwa ya ujenzi huo na kueleza kuwa,
Serikali imejipanga kuhakikisha hakuna mkandarasi atakayekwama kwa
sababu zozote zile.

Serikali
imedhamiria kuona hakuna mikwamo katika ujenzi huu, hivyo msirudishe
nyuma jitihada hizo, hakikisheni mnamaliza mradi huu kama
ilivyoelekezwa,” Alisisitiza Dkt.

 

 

 

 

 

 

 

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

You cannot copy content of this page