November 15, 2024

Waziri Jafo Ateta Na Wakuu Wa Mikoa

0

 

Waziri wa Nchi Ofisi ya
Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo ametoa rai kwa wakuu wa mikoa kuifanya ajenda ya usafi wa mazingira kuwa
ya kudumu.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu
wa Rais Mhe. Dkt. Selemani Jafo akizungumza wakati wa Mafunzo ya Uongozi kwa
Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala wa Mikoa yanayofanyika katika Shule ya
Uongozi ya Mwalimu Nyerere – Kibaha Mkoa wa Pwani tarehe 26 Agosti, 2023.

 Ametoa wito huo tarehe 26
Agosti, 2023 wakati akizungumza wakati wa Mafunzo ya Uongozi kwa Wakuu wa Mikoa
na Makatibu Tawala wa Mikoa yanayofanyika katika Shule ya
Uongozi ya Mwalimu Nyerere iliyopo Kibaha mkoani Pwani.

 Dkt. Jafo amewatakawakuu hao
wa mikoa kuzielekeza Mamlaka za Serikali za Mitaa zilizo chini
yao kusimamia vyema zoezi la usafiwa mazingira katika maeneo yao ili kuifanya
miji kuwa safi.

 Alisisitiza kuwepo na utaratibu maalumu wa kujisaidia
(kuchimba dawa) kwa abiria wanaosafiri kwa mabasi badala ya porini kama
unavyofanyika kwa baadhi ya mabasi hali inayosababisha uchafuzi wa mazingira.

 

Aidha, Waziri Jafo aliwataka wakuu wa mikoa hao kusimamia
suala la upangaji wa miji katika maeneo yao ili uwekezaji usikwame kutokana na
changamoto za kimazingira.

Alisema kuwa bila kupanga miji
vizuri uwekezaji unakuwa ni changamoto kubwa kwani itawalazima wawekezaji
kusubiri kupata Cheti cha Tathmini ya Athari kwa Mazingira (EIA) kabla ya
kuanza hatua ya ujenzi wa miradi.

 “Mtu atataka kujenga kiwanda
katika makazi ya watu, mambo yanakuwa yanaingiliana na mwisho wa siku wakati
mwingine EIA zinachelewa kwasababu tumeshindwa kufuata utaratibu wa mipango
miji hivyo, tuwasisitize watu wetu wa mipango miji kuhakikisha wanapanga vizuri
miji yetu kwa kushirikiana na Wizara ya Ardhi,” alisisitiza.

 Kwa
upande mwingine Waziri Dkt. Jafo aliwahimiza viongozi hao kuendelea kusimamia
zoezi la upandaji wa miti milioni 1.5 kwa mwaka katika kila halmashauri
wanazozisimamia ili hifahi ya mazingira iwe endelevu. 

 


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

You cannot copy content of this page