November 15, 2024

Waziri Mkuu Amuagiza Mchengerwa Kuchukua Hatua Za Kinidhamu Dhidi Ya Watumishi Waliofanya Ubadhilifu Kigoma

0

 

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amemuagiza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Mohamed Mchengerwa aende Kigoma na kuwachukulia hatua za kinidhamu watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma waliofanya ubadhirifu.



Alitoa agizo hilo jana (Ijumaa, Septemba 22, 2023) wakati akizungumza na viongozi wa dini, Serikali, Chama cha Mapinduzi (CCM) na watumishi wa Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma na Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma kwenye ukumbi wa NSSF, Kigoma mjini.


Akibainisha makossa yao kwenye kikao hicho, Waziri Mkuu alisema watumishi wa Halmashauri hiyo wanakabiliwa na matatizo mengi yakiwemo matumizi mabaya ya fedha, makusanyo kidogo sababu ya malumbano, mawakala kukaa na fedha mikononi badala ya kuzipeleka benki, matumizi ya fedha mbichi, Baraza la Madiwani kukosa taarifa za fedha na kutumia fedha za miradi kulipana posho.


“Kuna watu wamejilipa shilingi milioni 11 zikiwa ni posho ya safari ya Dodoma. Pia wametumia shilingi milioni sita kufanya service ya gari, hili ni gari la aina gani? Wengine wametumia shilingi milioni 9 kwenye sherehe za Siku ya Mtoto wa Afrika na wengine wamejilipa shilingi milioni 14. 8 kwenda kwenye sherehe za Nane Nane Tabora, hivi mlikaa siku ngapi huko?,” alihoji Waziri Mkuu.


Alisema anazo taarifa kwamba kuna tume ya TAMISEMI ilikwenda kufanya uchunguzi kwenye Halmashauri hiyo kuhusiana na matatizo hayo. Hivyo, akaitaka tume hiyo ikamilishe kazi yake haraka na kuwasilisha taarifa yao kwa Waziri Mchengerwa. “Tume ikamilishe kazi haraka, akabidhiwe Waziri. Ninamwagiza Mheshimiwa Waziri Mchengerwa akipokea taarifa ya tume hiyo, aje Kigoma achukue hatua,” alisema.


Waziri Mkuu amemaliza ziara yake ya siku tatu mkoani Kigoma na yuko mkoani Kagera kwa ziara ya siku tatu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

You cannot copy content of this page