Iramba Yakabidhi Mwenge Kibabe
MACHAL:MWENGE KUZINDUA MIRADI YA BIL. 1.7
Mkuu wa Wilaya ya Iramba Mkoani Singida (kushoto) akimkabidhi mwenge wa uhuru mkuu wa Wilaya ya Mkalama Mosses Machali (mfupi kushoto).
MKUU wa Wilaya ya Iramba Mkoani Singida,Selemani Mwenda ameahidi kutekeleza kwa wakati maagizo yaliyotolewa na kiongozi wa mbio za Mwenge Kitaifa Abdalla Shaib Kalm amesema kwa kurekebisha kasoro zilozoonekana katika baadhi ya Miradi iliyokqguliwa.Anaripoti Danson Kaijage,Mkalama.
Ametoa kauli hiyo leo tarehe 23 Septemba mwaka huu alipokuwa akikabidhi Mwenge wa uhuru kwa mkuu wa wilaya ya Mkalama Mosses Machali ili uweze kuendelea kuzindua miradi,kukagua na kuweka jiwe la msingi.
Mwenda amesema kuwa maelekezo ambayo yametolewa na kiongozi wa mbio za mwenge kwa maana ya kufanya marekebisho madogo ya miradi yatakamilishwa kwa muda mwafaka.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Mkalama Mosss Machali amesema kuwa mwenge unatarajia kuzindua na kutembelea miradi yenye thamani ya sh.Bilioni 1.7.
Hata hivyo Machali amesema kuwa lengo kubwa katika mbio za mwenge ni kuhakikisha miradi inayoendelea kutekelezwa kwa kiwango kinachotakiwa kwa kuzingatia thamani ya fedha.
Kwa upande wa kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa Abdalla Shaib Kaim,amesema lengo la Serikali kukagua miradi ni kubaini kama miradi inayotekelezwa inafikia kiwango kinacho kubalika.
Amesema ili kuwa na miradi endelevu na yenye kuwa kwenye kiwango ni vyema kutumia thamani ya fedha iliyokusudiwa kutokana na mradi ulivyotengewa hela.