November 15, 2024

KAMISHNA HIKI AFUNGUA KIKAO CHA WAKUU WA UPELELEZI WA MIKOA

0

Kamishna wa Uchunguzi wa Kisayansi, Kamishna wa Polisi Shaban Hiki amewapongeza Wakuu wa Upelelezi wa Mikoa kwa kazi kubwa wanayoifanya jambo ambalo limeendelea kuifanya Tanzania kuendelea kuwa shwari.

Kamishna HIKI ameyasema hayo leo Oktoba 11, 2024 wakati akifungua Kikao cha Wakuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai wa Mikoa (RCOs) na Vikosi kinachofanyika mkoani Dodoma ambapo pia Wakuu wa Vitengo vilivyopo Ofisi ya Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Makao Makuu ya Polisi Dodoma, wanashiriki.

“Watu wanaendelea na shughuli zao za uzalishajimali bila hofu hapa nchini na ninyi ni moja ya watu ambao mna mchango mkubwa katika hilo, hivyo, endeleeni kusimamia vyema masuala ya haki jinai katika maeneo yenu” Alisema Kamishna Hiki.

Kwa Upande wake Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai nchini, DCI Ramadhani Kingai ambaye ndiye Mwenyekiti wa Kikao hicho, amesema lengo la Kikao hicho ni kujadili na kujifunza mambo mbalimbali ambayo yataweza kuongeza weledi katika utendaji wa kazi za kila siku ambapo mada mbalimbali zitatolewa ikiwemo mada inayohusu Wajibu wa Jeshi la Polisi katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

You cannot copy content of this page