November 15, 2024

TANZANIA MWENYEJI JUKWAA LA TASNIA YA KUKU SADC

0

Kwa mara ya kwanza Tanzania imepata fursa ya kuwa mwenyeji wa mkutano wa jukwaa la tasnia ya kuku na ndege wafugwao kwa nchi wanachama kusini mwa Afrika SADC yaani Southen Africa Poultry Features Forum.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Oktoba 11,2024 jijini Dodoma Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Prof.Riziki Shemdoe amesema mkutano huo utafanyika tarehe 16 na 17Oktoba mwaka huu ktk ukumbi wa mlimani city jijini Dar es salaam ambapo mgeni rasmi atakuwa Naibu Waziri Mkuu Dkt.Doto Biteko.

Aidha Prof.Shemdoe amesema kuwa mkutano huo umelenga kujadili kubadilishana uzoefu Kutoka nchi za SADC pamoja na kubainisha fursa za kimkakati zinazohusu tasnia ya kuku na ndege wafugwao zilizopo katika nchi za SADC na kuweka maazimio yatakayoifanya tasnia hiyo iweze kuwa shindani jumuishi na kukua zaidi ili kuongeza fursa za masoko ndani na nje ya nchi za SADC kuongeza ajira kuinua mchango wa tasnia katika pato la taifa na kuchangia katika usalama na lishe

Hata hivyo Prof.Shemdoe amefafanua kuwa matukio yatakayoambatana na mkutano huo ni pamoja na maonesho ya bidhaa na huduma mbalimbali za wadau kutoka ndani na nje ya nchi.

“kutakuwa na vyumba rasmi kwaajili ya majadiliano ya kibiashara na fursa za kimkakati”amesema

Pia Prof.Shemdoe ameongeza kuwa mkutano huo umelenga kuonyesha fursa mbalimbali zilizopo katika mnyororo wa thamani wa kuku na ndege wafugwao..

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

You cannot copy content of this page