WAZIRI JAFO, BALOZI WA JAPAN WATETA USHIRIKIANO KATIKA HIFADHI YA MAZINGIRA
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhe. Dkt. Selemani
Jafo amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Japan hapa nchini, Mhe. Yasushi Misawa katika Mji wa Serikali,
Mtumba Jijini Dodoma.
Katika mazungumzo hayo yaliyofanyika leo Septemba
14, 2023 Dkt. Jafo amemshukuru Balozi Misawa kwa juhudi kubwa zinazofanywa na Serikali
ya Japan kupitia Shirika la Kimataifa la Maendeleo (JICA) kwa kuendelea
kufadhili miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo maji, elimu, barabara, afya na
kuiomba Serikali hiyo kusaidia pia miradi ya uhifadhi na usimamizi wa mazingira
iliyopo nchini.
Waziri Jafo amemueleza Balozi Misawa kuwa ajenda ya
mazingira ni moja ya kipaumbele muhimu vilivyopewa msukumo na Serikali ya Awamu
ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ambapo Serikali kupitia
Ofisi ya Makamu wa Rais imeendelea na juhudi za kuhamasisha jamii kutumia
nishati mbadala ili kuhamasisha uhifadhi na utunzaji mazingira nchini.
“Tanzania tunazalisha takribani tani
Milioni moja za taka ngumu ambazo ni fursa ya uzalishaji wa nishati mbadala…tunatumia
asilimia 30 tu ya nishati hiyo…Tunahitaji nishati hii kwa ajili ya matumizi ya
kijamii na kiuchumi. Tunahitaji wawekezaji wengi zaidi kujitokeza kwa ajili ya
uwekezaji,” amesema Mhe. Dkt.Jafo.
Amesema kuwa Serikali imeweka mazingira wezeshi na rafiki
kwa wawekezaji na wadau wa nishati hiyo kuweza kujitokeza na kushirikiana na Serikali katika kutekeleza miradi mbalimbali ya nishati mbadala hususani katika maeneo ya vijijini ili kuongeza
upatikanaji wa nishati mbadala ya kupikia.
Waziri Jafo pia amemhakikishia Balozi Misawa
ushirikiano na utayari wa Serikali ya Tanzania katika kuhakikisha utekelezaji
wa miradi ya nishati jadidifu
ikiwemo jotoardhi, tungamotaka, upepo na jua pamoja na matumizi bora ya Nishati mbadala ili kuleta manufaa
kwa wananchi na jamii kwa ujumla.
Akifafanua zaidi Waziri Jafo amesema Serikali
kupitia Ofisi ya Makamu wa Rais imeandaa sera, kanuni na miongozo mbalimbali ikiwemo
ikiwemo katazo
Kwa taasisi zote za umma na binafsi kwa upande wa Tanzania Bara zinazoandaa
chakula na kulisha watu zaidi 300 kusitisha matumizi ya mkaa na mkaa ifikapo
mwaka Januari 2025.