WAZIRI JAFO AKISHIRIKI MKUTANO WA AGRF
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muunganona ,Mazingira)
Mhe. Dkt. Seleman Jafo amesema Serikali imewekeza katika teknolojia ya kilimo kinacho milimabadilikoya tabia nchi kupitia miradi ya mazingira inayotekelezwa nchini.
Dkt. Jafo amesema hayo alipochangia mjadala wakati wa Mkutano wa Jukwaa
la Mifumo ya Chakula Afrika (AGRF) unaofanyika katika Kituo cha Kimataifa cha
Mikutano cha Julius Nyerere jijini Dar es Salaam leo Septemba 08, 2023.
Ametoa wito kwa nchi zilizoendelea kuunga mkono juhudi hizo za Serikali kwa
kufadhili miradi ya kilimo inayotekelezwa nchini ilipawepo na tija na uhakika wa chakula.
Kutokana na Makubalianoya Paris kuhusu nchi zilizoendelea kuchangia fedha kwa mataifa ya nayoendelelea katika kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabia nchi,
Waziri Jafo alipendekeza kupitia fedhahizo pia pawe na mafungu maalumu ya kuwezesha kilimo cha
kuhimili mabadiliko ya tabia nchi.
Aidha, Wazir iJafo alisema ilikukabilianana changamoto ya ukame unaosababishwa na uhaba wa mvua katika baadhi ya maeneo Serikali imewekeza zaidi ya shilingi bilioni
200 kwa ajili ya uchimbaji wa malambo 114 ya umwagiliaji.
“Tunafahamu sekta ya kilimo inaathirika sana kwa maana mvua hazitoshi hivyo miradi ya adaptation ni muhimu sana kama nchi hizo zikiwekeza katika teknolojia ya kilimo.
Tuipongeze Serikali inayoongozwa na Rais Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu
Hassan kupitia Wizara ya Kilimo kwa kuja na Mradiwa BBT kwa vijana na tunaona umeanza kutimiza ndoto za vijana,”
alisema.
Aidha, Katika kuhakikisha kilimo kinakuwa na tija pamoja na kuwepo kwa changamoto za kimazingira,
Dkt. Jafo alisema Serikali inaimarisha uzalishajiwa nishati ikiwemo mradi wa Bwawa la
kufua umeme la Mwalimu Nyerere nakusambaza umeme vijijini.
Alifanua kuwa hatua ya usambazaji nishati vijiji itasaidia kuwavutia wawezekaji kufungua
viwanda vya uchakataji wa mazao na hivyo kukuza uchumi kwa kuuza bidhaa zilizochakatwa badala ya mazao malighafi.
“Katika mkutano huu tumewataka wenzetu watimize wajibu wao kuchangia fedha za kusaidia nchi zinazoendelea katika miradi ya kuhimili mabadiliko ya tabia nchi hasa kwenye smart agriculture kwani mvua hazitoshi
kilimo,”
alisisitiza Waziri Jafo.