November 14, 2024

ASKOFU DK.RUTTA AKEMEA ROHO YA VISASI

0

 ASKOFU mkuu wa Kanisa la Glory to God Ministry (GGM) lenye makao makuu yake Maili mbili Jijini Dodoma Dk.Benson Rutta amewaonya  watanzania pamoja na watawala kuachana na roho ya kulipiza kisasi pale wanapokosolewa au kupinga mawazo yao.Anaripoti Danson Kaijage,Danson Kaijage,Dodoma (Endelea).


Ametoa onyo hilo leo Jumapili tarehe 17 September kwenye ibada maalumu iliyolenga kuwafundisha waumini na watanzania kwa ujumla kuachana na tabia ya kulipiza kisasi pale mtu anapokuwa amekosewa au kupinga mawazo ya mtu ambaye anapinga mawazo ya mwingine.


Askofu Dk.Rutta amesema kuwa kitendo cha mtawala au kiongozi yoyote au mtu mwingine kulipiza kisasi kwa mtu mwingine kutokana nankupingwa kwa mawazo yake yanaweza kusababisha uaribifu au machafuko katika eneo husika.


Kiongozi huyo ambaye awali alikuwa askofu wa kanisa la Full Gospel Bible Fellowship wilayani Kondoa na kujiengua na kuanzisha huduma ijulikanayo kwa jina la Glory to God Ministry yenye makao yake jijini Dodoma amesema hakuna haja ya kulipiza kisasi kwa mtu ambaye amekukosea.



Askofu huyo ambaye amekuwa akihubiri upendo,amani na utulivu kwa Watanzania pamoja na mataifa mengine amesema machafuko yanaweza kutokea kutokana nankulipiza kisasi na wakati huo huo amani na utukufu na baraka zinaweza kutawala kutokana nankusamehe pale unapokuwa umepingwa kwenye mawazo yako.


“Napenda kuwakemea viongozi mbalimbali pamoja na watawala kuacha mara moja kulipiza kisasi pale inapotokea watu wakapingana na mawazo yenu,au wanapotoa mawazo yao ambayo yanaweza kuwa na ustawi katika eneo husika.


“Kulipiza kisasi kunaweza kuliangamiza kaifa na wakati mwingine,kumfanya uliyemkosea afanikiwapo wewe uliyemtesa ukawa mtumwa kwake na kujihisi kuwa haufai mbele za Mungu au mbele za watu.


“Tumkumbuke Yusufu alivyouzwa na ndugu zake,haitoshi akasingiziwa na mke wa mfalme Yerode na kutupwa gerezani lakini kwa kuwa Yusufu hakulipiza kisasi matokeo yake Mungu alimwinua Yusufu na kumfanya kuwa Waziri Mkuu katika taifa la Misri wakati yeye akiwa ni mtu kutoka mchi ya Israel”ameeleza Askofu Dk.Rutta.



Mbali na hilo Askofu Dk.Rutta amewataka waumini wa kanisa hilo kuhakikisha wanafanya kazi kwa bidii kwa nia ya kujiongezea kipato kwa nia ya kumtolea Mungu na kujiongezea kipato chao wenyewe na kwa taifa.


Kiongozi huyo wa Kiroho amewataka Wakristo wenye uchumi mzuri kuwekeza kwenye miradi mikubwa kwa nia ya kuinua pato la mtu mmoja mmoja na jamii kwa ujumla wake.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

You cannot copy content of this page