November 15, 2024

BUCKREEF YAJIVUNIA KUSIMAMIA VYEMA SHERIA YA LOCAL CONTENT

0

Na Prosper Makene, Geita
Kampuni ya Uchimbaji Dhahabu ya Buckreef (BGC) imesema kuwa inajivunia kutekeleza kwa vitendo sera ya ushirikishaji watanzania na kuwanufaisha kupitia mnyororo wa uwekezaji katika sekta ya madini (Local content).
Akiongea katika maonesho ya kimataifa ya saba ya teknolojia ya madini yanayoendelea katika viwanja vya EPZA Bomba Mbili mjini hapa, Meneja Mkuu wa Kampuni hiyo, Mhandisi Gaston Mjwauzi amesema kuwa Kampuni ya Buckreef ambayo ni ubia kati ya serikali ya Tanzania, yenye hisa asilimia 45 kupitia STAMICO na Kampuni ya TRX yenye hisa asilimia 55 ya Canada, imetekeleza kwa kiasi kikubwa sheria ya local content ambapo utekelezaji wake ni zaidi ya asilimia mia.
“Tumeweza kutekeleza vyema maagizo yote yaliosemwa kwenye sheria ya local content kama ilivyoainishwa chini ya Kifungu cha 102 cha Sheria ya Madini Sura ya 123 na Kanuni za Madini (Local Content), 2018 kama ilivyorekebishwa mwaka 2019,” alisema.
Aliongeza: “Tunajivunia kuufahamisha umma kwamba, angalau asilimia 100 ya wafanyakazi wetu ni Watanzania, na tuko mstari wa mbele katika kufanya kazi kwa usawa na makampuni ya ndani.”
Alisisitiza kuwa Kampuni kwa miaka michache ijayo, Kampuni hiyo ipo kwenye utekelezi wa malengo makubwa ya kuwa moja ya makampuni ya madini yenye mchango mkubwa kwenye uchumi wa nchi.
“Wakati tunaanza uchimbaji dhahabu miaka kadhaa nyuma katika Kijiji cha Mnekezi eneo la Lwamgasa Mkoani Geita tulikuwa na mtambo mmoja wenye uwezo wa kuchakata dhahabu tani 15 kwa saa, lakini hivi sasa Kampuni yetu imekuwa kwa kiasi kikubwa ambapo hivi sasa tuna uwezo wa imekua kusindika zaidi ya tani 100 kwa saa,” alisema.
Akizingumza mashirikiano yao na jamii kwenye upande wa CSR, Mhandisi Mjwauzi alisema kuwa kampuni yao imekuwa ikitenga kila mwaka fungu kwa ajiri ya kusaidia jamii inayowazunguka kwenye maeneo ya afya, elimu na maji ili kuhakikisha wananchi wanapata wa kupata huduma muhimu za kijamii.
“Kila mwaka, kwa kawaida tunatengwa kati ya 420m/- na 450m/- kwa ajili ya kusaidia sekta zilizotajwa,” alisema.
Kwa bajeti hiyo, alisema Kampuni hiyo hadi sasa imeweza kujenga vituo kadhaa vya afya, madarasa, na visima vya maji katika maeneo mbalimbali ya jamii inayowazunguka.
Alisema Kampuni ilianza kazi ikiwa na wafanyakazi 50 pekee, lakini leo imeajiri zaidi ya wafanyakazi 700, jambo ambalo limefungua fursa zaidi za ajira kwa Watanzania na hivyo kuboresha maisha yao.
Aliipongeza serikali kwa kuweka sera nzuri za kukuza uchumi wa sekta hiyo.
Kwa upande wake, Meneja Rasilimali Watu Kampuni hiyo, Melda Msuya, alisema kampuni hiyo imefanikiwa kuongeza idadi ya wafanyakazi wa kike kutoka watatu walipoanza hadi 25.
Alisema kampuni inaajiri wafanyakazi huku ikiakisi sera ya kusaidia jinsia ya kike kwa kuzingatia sifa zinazohitajika za kitaalamu na uwezo.
Msuya amempongeza Rais Dtk Samia Suluhu Hassan kwa kuweka mazingira wezeshi ya kuruhusu wanawake kushiriki kikamilifu katika sekta ya madini.
MWISHO

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

You cannot copy content of this page