November 14, 2024

CCM yajiapiza kujenga Hospitali ya Rufaa Mikoa ya Shinyanga, Iringa na Pemba

0

 Na Paul Kayanda, Kahama

JUMUIYA ya wazazi ya chama cha mapinduzi, CCM, Taifa inatarajia kutekeleza miradi mikubwa ya maendeleo kwenye sekta ya afya kwa kujenga, hospitali maalumu za Rufaa, katika Mikoa ya Shinyanga, Iringa na Pemba visiwani Zanzibar zenye lengo la kutoa huduma za kibingwa ikiwa ni utaratibu wa jumuiya hiyo kuwekeza katika miradi ya kijamii Nchini.

 


Mwenyekiti wa Wazazi wa CCM taifa, Rajab Fadhili Maganya amesema hayo jana alipotembelea ofisi za CCM Mkoa wa Shinyanga na Kahama  baada ya kupokelewa na viongozi wa jumuiya ya chama na serikali.

Akiwa katika Manispaa ya Kahama Mkoani humo  alipotembelea eneo la nzongomela lenye ukubwa wa zaidi ya ekari 50 lililotengwa kwa ajili ya mradi wa ujenzi wa hospitali hiyo kubwa na yakisasa pamoja na Chuo cha Afya mwenyekiti alitoa maelekezo kwa cha na Serikali kuhakikisha kuwa mradi huo haukwami.

“Tuna miradi mikubwa mitatu tunataka tujenge hospitali ya kisasa lakini tunaanza hapa Kahama tunajenga Hospitali yenye uwezo wa kubeba vitanda kuanzia 1200 mpaka 1500  na vitengo vyote vinavyofahamika vyate vya hospitali,”alisema Mwenyekiti CCM Taifa Rajab Fadhili Maganya.    



Naye mwenyekiti wazazi CCM Mkoa wa Shinyanga John Siagi, alisema kuwa Mradi huo unatekelezwa katika Mkoa wa Shinyanga Manispaa ya Kahama umekuja kwa muda mwafaka ukilinganisha na mwingiliano mkubwa wa wananchi na ni Mji ambao unakua kwa kasi kubwa sana ukilinganisha na kwamba Kahama ni kitovu cha biashara na ni lango kuu la kwenda Mikoa jirani ya Rwanda, Burundi Uganda na Congo Drc.


“Tunaimani katika uwekezaji huu ambao utakuwa na tija kwa jamii na wana Shinyanga na itahuhudumia wananchi wa Miko mingine ya Geita, Tabora Wilaya zake lakini itakuwa ni sehemu ya kupunguza mrundikano wa wagonjwa katika Hospitali ya Manispaa ya Kahama inayofanya kazi sasa,” alisema.

Kwa upande wake, Mkuu wa wilaya ya Kahama, Mboni Mhita licha ya kuipongeza Jumuiya ya wazazi ya chama cha mapinduzi, serikali imetenga eneo hilo kwa lengo kusogesa huduma hiyo ya afya kwa wananchi wa Mkoa mzima wa Shinyanga.

“Eneo hili kuna ekari 25 kwaajili ya chuo lakini kuna ekari 28 kwaajili ya ujenzi wa Hospitali kubwa nay a kisasa yote ni maandalizi ya sisi kama wana Kahama kwaajili ya kupokea mradi huu mkubwa wenye nia ya kutatua changamoto mbalimbali ambao ilani ya chama cha mapinduzi iliahidi na serikali ipo mstari wa mbele kutekeleza,” alisema Mboni Mhita Mkuu wa Wilaya ya Kahama.

Thomas Muyonga, ni  Mwenyekiti wa CCM, Wilaya ya Kahama ambapo naye alieleza kuwa kama chama Wilaya wanayofuraha kubwa kupokea mradi huo kwamba mahitaji ya Hospitali maeneo hayo ni makubwa, manispaa hiyo kwa sasa inawatu wengi kwa maana hata majimbo matatu ya Uchaguzi Ushetu, Msalala na Kahama yenyewe yanawatu wengi.

Muyonga alitumia mwanya huo kuwaomba wananchi bila kuja itikadi yoyote ya vyama vyao wapokee mradi huo kwani utakapokamilika umelenga kutatua changamoto na kelo mbalimbali kwa wananchi licha ya kuwepo hospitali kubwa nay a kisasa ya manispaa ya Kahama.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

You cannot copy content of this page