DKT. MPANGO: “BILIONI SABA KUJENGA STENDI KUU YA MABUS IGUNGA”
? Soko Kuu la Kati kufanyiwa maboresho.
?Kiwanda cha Kuchambua Pamba kujengwa Mbutu, Igunga.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isidor Mpango amewahakikishia Wakazi wa Jimbo la Igunga kuwa Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan itatoa Fedha Shilingi Bilioni Saba kwa ajili ya ujenzi wa Stendi ya Mabus kubwa ya kisasa kufuatia ombi la Mbunge wa Jimbo la Igunga Mhe. Nicholaus George Ngassa wakati wa ziara ya kikazi ya Mheshimiwa Makamu wa Rais kwenye Wilaya ya Igunga Leo tarehe 8 Oktoba, 2024.
Aidha Mhe. Ngassa (MB) ameomba ujenzi wa Soko Kuu la Kati, kukamilishwa kwa miradi ya maji na barabara ambayo imepata wakandarasi, ujenzi wa Ofisi ya Halmashauri ya Wilaya, Changamoto ya Tembo kuvamia makazi ya Wananchi.
Katika ziara ya Makamu wa Rais, Waziri wa Kilimo Mhe. Hussein Bashe (Mb) amesema kwasasa Wizara ya Kilimo imeanza mchakato wa ujenzi wa Kiwanda cha Kuchambua Pamba baada ya kupatiwa eneo na Halmashauri ya Wilaya ya Igunga, aidha Waziri Bashe (Mb) katoa kauli kuhusu maboresho ya Skimu ya Umwagiliaji ya Mwamapuli (Mwanzugi) ambapo Bilioni Ishirini (Tshs. 20,000,000,000/=) zitatumika.