November 15, 2024

IAA YADHAMIRIA KUFANYA MAKUBWA MWAKA WA FEDHA 2023/2024

0

Na Mwandishi wetu Arusha 


Mkuu wa Chuo Cha Uhasibu Arusha (IAA) Prof. Eliamani Sedoyeka leo tarehe 15 Septemba 2023 ametoa rasmi ripoti ya utendaji kazi ya mwaka wa fedha 2022/2023 na kueleza mipango na mikakati ya mwaka mpya wa fedha 2023/2024.

Akizungumza na waandishi wa habari leo katika kampasi ya Arusha, Prof. Sedoyeka ameeleza kuwa IAA imepata mafaniko makubwa kutokana na juhudi wanazozifanya ikiwemo; kuboresha mazingira ya kujifunzia (Miundombinu), kuongeza mitaala mipya ambayo mpaka sasa imefikia 71 kwa ngazi zote kwa mwaka wa masomo 2023/2024.


Aidha, ameongeza kuwa IAA imefanikiwa kuongeza idadi ya wanafunzi kutoka 10,342 mwaka 2021/2022 mpaka 13,716 kwa mwaka 2022/2023, ongezeko hilo likienda sambamba na ongezeko la mapato ya ndani kutoka bilioni 15 mwaka 2021/2022 mpaka kufikia 2022/2023. 


Katika hatua nyingine Prof. Sedoyeka ameeleza kuwa IAA inaendelea kuweka jitihada katika kuhakikisha inakuwa na wataalam (wahadhiri) wa kutosha ili kuendana na ongezeko la wanafunzi; ambapo mpaka sasa jumla ya watumishi 52 wanasoma shahada ya uzamivu (PhD) katika Vyuo Vikuu mbalimbali vya ndani na nje ya nchi na watumishi Tisa (09) wanasoma  shahada ya uzamili (Masters)

Kuhusu ushirikiano na wadau Profesa Sedoyeka amesema IAA itaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali ambapo kwa mwaka 2022/2023 imeanzisha rasmi ushirikiano na Jeshi la Polisi katika kutoa mafunzo kwa kozi mbli za Shahada ambazo ni Bachelor Degree in Cyber Security, Bachelor Degree in Security and Strategic Studies na Kozi mbili za Shahada ya Uzamili ambazo ni Master of Information Security na Master of Arts in Peace and Security Studies.


Sanjari na hili ameongeza kuwa Chuo kitaendelea kuongeza mitaala kulingana na mahitaji ya wakati na kuboresha iliyopo kuendana na mahitaji ya Taifa na soko la ajira ili wataalam watakaondaliwa na Chuo cha Uhasibu Arusha waweze kuwa chachu katika kutatua changamoto za kijamii na kiuchumi kwa jamii na Taifa kwa ujumla.

Prof. Sedoyeka ameishukuru serikali ya Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, inayoongozwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kutokana na kazi kubwa wanayoifanya ambayo ina mchango mkubwa katika maendeleo ya chuo, katika kuhakikisha IAA inatoa elimu bora kwa jamii ya Watanzania.


Vile vile, Prof Sedoyeka amefafanua mipango mikakati waliyonayo kwa mwaka mpya wa fedha ambayo ni pamoja na ujenzi wa kituo cha kimkakati cha TEHAMA, kukamilisha ujenzi wa baadhi ya majengo ya madarasa na hosteli za wanafunzi katika kampasi ya Arusha, kukamilisha ujenzi wa Kampasi ya Babati na Dodoma, pamoja na ujenzi wa kampasi mpya ya Songea.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

You cannot copy content of this page