M/Kiti Halmashauri Msalala apongeza watendaji kuvuka lengo kuvuka lengo la makusanyo.
Na Paul Kayanda, Kahama
MWENYEKITI wa Halmashauri ya Msalala Wilayani Kahama, Mkoani Shinyanga
Mibako Mabubu amepongeza ushirikiano kati ya watendaji wa Halmashauri hiyo
pamoja na Madiwani wake kwa kuvuka lengo la makusanyo ya mapato jambo
ambalo itakuwa ni mfano wa kuigwa hapa nchini.
Mwenyekiti huyo amesema kuwa mahesabu ya Halmashauri ya Msalala yamekwenda vizuri chini ya Ofisi ya mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo pamoja na timu yake kwa kushirikiana na madiwani.
Amesema kuwa hiyo ni kutokana na jitihada mbalimbali ikiwemo kupunguza hoja kwa usimamizi mzuri pamoja na kupunguza madeni makubwa kama lile la zaidi ya Bilioni 4 walizokuwa wakiudai Mgodi mkubwa wa Dhahabu wa Bulyanhulu uliopo Kakola.
Mwenyekiti Mibako Mabubu ameyasema hay oleo Augost 30 kwenye kikao cha maalumu cha baraza la madiwani cha kupitia mahesabu ya mwaka 2022/2023 kilichofanyika katika ukumbi wa Halmashauri hiyo uliopo Kata ya Ntobo Halmashauri ya Msalala Wilayani Kahama Mkoani hapa.
Aidha Mwenyekiti huyo ameitaka Ofisi ya Mkurugenzi kuendelea kusikiliza ushauri wa Madiwani pamoja na kukaza uzi huo huo ili kuendelea kupata hati safi na kuwa Halmashauri bora kwa ukusanyaji wa mapato kuliko Halmashauri
Nyingine nchini.
Hata hivyo Afisa serikali za mitaa Baraka Bulongo pamoja na katibu wa itikadi na uenezi Wilaya ya Kahama Joachim Simbila wamepongeza hatua ya ushirikiano huo na kwamba hiyo taarifa imejadiliwa kuanzia vikao vya menejimenti, vikao vya kamati ya ukaguzi pamoja na vikao vya fedha na kuongeza kuwa kama kuna mapungufu walekebishe kabla ya kufika kwa CAG.
Pia wamesema kuwa chama kiliwatuma kusimamia vizuri shughuli za maendeleo kwa wananchi, na kwamba kwa hatua hiyo madiwani pamoja na watendaji wa halmashauri hiyo wanastahili pongezi kwa kazi kubwa wanayoifanya.
“Muendelee kutatua changamoto zinazotetolewa na wananchi, niwaombee kwa mwaka mpya wa fedha unmnaokuja muendelee kufanya vizuri na mjue kuwa wananchi wanahitaji matokeo mazuri na siyo vinginevyo,” amesema Simbila katibu wa itikadi na uenezi Wilaya Kahama.
Hata hivyo Matrida Musoma Diwani wa Kata ya Ikinda pamoja na Benedicto Manwari Diwani wa Kata ya Lunguya wamesema kuwa wanaimani na watendaji wa halmashauri hiyo na watazidi kushirikiana nao ikiwemo kutoa ushauri kwa watendaji hao ili kutekeleza miradi mbalimbali za maendeleo kwa wananchi.
“Leo ilikuwa ni siku ya kikao chetu,cha 2022/2023 ambacho mwisho kilikuwa kinaishia mwezi juni na leo tumepokea taarifa hii kwa mikono miwili, lakini halmashauri ilitununulia vishikwambi na kututumia taarifa hiyo mapema ili mjumbe aweze kuipitia na kupata cha kusema kwa hiyo mimi nimeisoma kuanzia nyumbani mpaka leo kwa hiyo mhasibu alipokuwa anawasilisha alikuwa kama anairudia tu,” amesema Manwali Diwani Kata ya Lunguya.