MAAFISA KILIMO WA WAKALA WA MBEGU WATAKIWA KUHAKIKISHA WANAONGEZA UZALISHAJI WA MBEGU BORA
Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Mbegu za kilimo (ASA) Bwn. Leo Mavika amewataka Maafisa Kilimo wa Wakala wa Mbegu za kilimo kuhakikisha wanaongeza Uzalishaji wa Mbegu bora za kilimo ili kuweza kufikia Malengo yaliyowekwa na serikali.
Amesema hayo wakati akifungua Mafunzo ya Siku Tatu ya Technolojia za Uzalishaji wa Mbegu bora za kilimo kwa maafisa kilimo wa ASA Mkoani Dodoma yanayotrkelezwa kupitia programu ya kuendeleza kilimo na Uvuvi – AFDP.
“Watumishi wote waliohudhuria Mafunzo hayo wanapaswa kuzingatia Elimu itakayotolewa na wataalam ili kuleta ufanisi kwenye mashamba ya Taasisi. ASA inajukumu kubwa la kuhakikisha inazalisha Mbegu bora Kwa wingi ili kukidhi mahitaji ya Nchi na kuepuka kuagiza Mbegu za kilimo kutoka Nje ya Nchi” Bw. Mavika
Aliendelea na kusema “ Wakala wa Mbegu za kilimo ASA ina kipaumbele cha kuzalisha mbegu za Mazao 13 ambazo zinapaswa kupatikana wa wingi ikiwepo zao la Mahindi, Alizeti,Mpunga pamoja na Mazao mengine” Bw. Mavika
Pia, Kaimu Mtendaji Mkuu Mavika amesema Wakala wa Mbegu za kilimo ASA inatakiwa kuchangia kwa sehemu kubwa uzalishaji wa Tani 127,650 ambazo ndio mahitaji halisi ya Nchi.
Aidha amesama Malengo ya Taasisi ni kuona mabadiliko makubwa baada ya Mafunzo hayo katika Mashamba kutokana na kupewa Mafunzo bora ya Uzalishaji wa Mbegu kwa Technolojia za kisasa kutoka kwa wataalamu waliobobea watakaowasilisha mada.
Bwn, Mavika amepongeza Mafunzo hayo ya Programu ya kuendeleza kilimo na Uvuvi -AFDP yatasaidia kukuza uelewa kwa watumishi nakusaidia kufikia Malengo.
Aidha kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Biashara Emmanuel Maziku amesema Mradi huo unatekelezwa kwenye Mashamba matatu ambayo ni Shamba la Kilimi Nzega pamoja na Shamba la Msimba Kilosa Mkoani Morogoro.
Amesema Mradi huo unatekeleza mambo mbalimbali kama vile karakana,majengo ya ofisi,Ukarabati wa Nyumba za watumishi,ujenzi wa Ghala la kuhifadhia Mbegu Kilimi pamoja na kununua Mtambo wa kuchakata Mbegu.
Aidha amesema baadhi ya Malengo ya Mradi huo nikuongeza Uzalishaji wa Mbegu pamoja na kuhamasisha sekta Binafsi kuzalisha Mbegu bora za kilimo.