November 14, 2024

Makamu Wa Raisi Azungumza Na Taasisi Ya Wafanyabiashara Marekani

0

 

Makamu wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango amesema serikali ya Tanzania ina dhamira ya dhati
ya kushirikiana na kufanya kazi kwa karibu na jumuiya ya wafanyabiashara wa
ndani ya nchi na wale wa kimataifa ili kukuza uwekezaji wa sekta binafsi.

 


Makamu wa Rais amesema hayo wakati alipofanya
mazungumzo na Taasisi ya
Kimkakati kwa Biashara
za Kimataifa na Serikali ya nchini Marekani (BCIU), mazungumzo yaliyofanyika
Jijini New York. Amesema nchini Tanzania sekta binafsi ni mshirika mkuu wa
maendeleo na taifa lipo tayari kwaajili ya biashara hivyo amewakaribisha
wafanyabishara hao kuwekeza Tanzania na kutumia fursa zilizopo ili kuiwezesha
nchi kufanikisha malengo ya maendeleo endelevu (SDGs).

 

Makamu
wa Rais amesema Tanzania ni nchi yenye mazingira mazuri zaidi ya uwekezaji
kusini mwa jangwa la sahara ikiwa na kasi ya ukuaji kiuchumi, amani,
miundombinu ya nishati kutoka katika vyanzo mbalimbali, ardhi ya kutosha ya
kilimo na hali ya hewa rafiki, kuimarishwa kwa mtandao wa usafiri na
usafirishaji ikiwemo ujenzi wa reli ya kisasa pamoja na huduma nyingi
zinazovutia uwekezaji na biashara.

 

Makamu wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango
akifanya mazungumzo na Taasisi ya Kimkakati kwa Biashara za Kimataifa na Serikali ya nchini Marekani
(BCIU), mazungumzo yaliyofanyika Jijini New York.

Halikadhalika
Makamu wa Rais amesema Tanzania inawakaribisha wawekezaji katika sekta
mbalimbali ikiwemo sekta ya afya kama vile ujenzi wa viwanda vya uzalishaji wa
vifaa tiba na dawa kwa kuzingatia uwepo wa soko katika ukanda nchi za Jumuiya
ya Maendeleo Kusini Mwa Afrika (SADC), kuwekeza katika kilimo, nishati,sekta ya
usafiri na usafirishaji pamoja na miundombinu ya tehama.

 

Pia amewakaribisha kutumia vema ukuaji wa sekta ya
viwanda vya ngozi ikizingatiwa Tanzania ni nchi ya pili kwa idadi kubwa ya
mifugo barani Afrika. Pia amesema Tanzania ni nchi ya nne barani Afrika kwa
uzalishaji mkubwa wa pamba (baada ya Mali, Burkina Faso, na Misri) na nchi ya
nne kwa uzalishaji wa pamba asilia Duniani (baada ya India, China, na Uturuki).
Amesema kwa sasa uwezo wa usindikaji wa pamba umeongezeka na kwa sasa
zinasafirishwa nguo hadi nchini Marekani chini ya mpango wa AGOA.



Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akifanya mazungumzo na Taasisi ya Kimkakati kwa Biashara za Kimataifa na Serikali ya nchini Marekani (BCIU), mazungumzo yaliyofanyika Jijini New York.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

You cannot copy content of this page