November 14, 2024

MANISPAA YA MOSHI KUONGEZA NGUVU KATIKA VIKUNDI VYA VIKOBA UTOAJI WA ELIMU YA CHANJO.

0

Na. Elimu ya Afya kwa Umma

Katika kuhakikisha huduma za chanjo zinafanikiwa kwa ufasaha na kuleta tija katika jamii, Manispaa ya Moshi Mkoani Kilimanjaro imesema ipo tayari kuongeza nguvu utoaji wa elimu ya afya kuhusu chanjo  katika vikundi vya kukopa vya akina mama ari maarufu VIKOBA.

Akizungumza katika wakati akifunga Mafunzo ya siku 4 ya kuijengea uelewa jamii umuhimu wa kuimarisha huduma za chanjo (HCD)Mstahiki Meya wa Manispaa ya Moshi Mkoani Kilimanjaro Zuber Abdallah ameonesha kufurahishwa na namna mafunzo hayo yanavyoshirikisha jamii moja kwa moja kwa kutumia ubunifu, hivyo ameridhia kuyapokea mawazo yaliyotokana na mafunzo hasa kutumia VIKOBA na kuja na mkakati wa mifumo utakaosaidia akina vituo vya kutolea huduma za afya kusomana ili kurahisisha uratibu wa huduma za chanjo.

“Niwapongeze sana Wataalamu kutoka Wizara ya Afya na Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam kwa kuja na ubunifu huu wa kushirikisha jamii moja kwa moja kuanzia hatua za mwanzo hadi mlaji wa mwisho, hivyo niwaahidi kwa kuwatumia akina mama  katika vikundi vya kukopa (VIKOBA)tutaifikia jamii kwa  wingi zaidi na kinachotakiwa tu kwa sasa ni kuhakikisha tunashirikiana katika kuhakikisha tunakuwa na mfumo unaoweza kusomana kutoka kituo kimoja cha huduma za afya hadi kingine, naomba sana hili mtusaidie”amesema.

Kwa upande wake Simon Nzilibili kutoka Wizara ya Afya, Sehemu ya Elimu ya Afya kwa Umma, Simon Nzilibili amesema zaidi ya mikakati 300 .

“Zaidi ya mikakati 300 imependekezwa ikiwemo  kuyatumia majukwaa ya akina mama kupitia VIKOBA na pia suala la mifumo ambalo litarahisisha takwimu kusomana nah ii itarahisisha kuongeza hamasa ya chanjo na nitoe wito kwa wananchi kuendelea kuwapeleka watoto kupata chanjo”amesema.

Kwa upande wake, Salome Mwinjuma kutoka Mpango wa Taifa wa Chanjo, Wizara ya Afya amesema mtoto asiyepata chanjo anaweza kupata madhara mbalimbali ikiwemo ulemavu wa macho na viungo vingine vya mwili.

Kwa upande mwezeshaji wa mafunzo ya HCD kutoka chuo Kikuu cha Dar Es Salaam  Dkt. Joseph Mushi amesema mfumo umekuwa na mchango mkubwa katika kuleta ubunifu wa utatuzi wa matatizo kwa kushirikisha jamii.

Nao baadhi ya Wanufaika wa Mafunzo hayo ya HCD wakiwemo Viongozi wa dini, viongozi wa jamii na Wazee wa Kimila wamesema  ni muhimu jami kutambua umuhimu wa chanjo katika kuleta ustawi wa jamii.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

You cannot copy content of this page