MCHUNGAJI AWATAKA VIONGOZI KUHESHIMU SHERIA ZA NCHI NA KUTENDA HAKI
Na Danson Kaijage,Dodoma.
MCHUNGA Kiongozi wa kanisa la Tanzania Assembles of God TAG RCC Ihumwa Dodoma,Lameck Siliti amewataka watanzania wote pamoja viongozi mbalimbali kwa kuhakikisha wanaheshimu sheria za nchi pamoja na kusimamia haki.
MCHUNGA Kiongozi wa kanisa la Tanzania Assembles of God TAG RCC Ihumwa Dodoma,Lameck Siliti aliyevaa shati la kitenge akiwaombea waumini wa Kanisa hilo.
Mchungaji Siliti ametoa kauli hiyo kwenye ibada iliyofanyika kanisani hapo ilyokuwa imebeba ujumbe zaidi wa kuzingatia na kuheshimu sheria za Kimungu na watu kuishi kwenye utakatifu na kupendana.
Kiongozi huyo wa Kiroho alisema kuwa ili kuwa na nchi yenye ustawi ni lazima iwe na watu ambao wanazingatia sheria za nchi pamoja na sheria za Kimungu na kwa kufanya hivyo hakuna mtu ambaye atamuonea mwingine.
“Hakuna kiongozi yoyote ambaye anaweza kuongoza vizuri kama hatafuata sheria za nchi husika na kama kila mtu atazingatia sheria zilizowekwa na nchi husika hakika kila mtu atamuona mwenzake kuwa ni muhimu.
“Lazima kuzingatia sheria za nchi na kuzitii na hakuna kiongozi yoyote ambaye anaweza kuongoza bila kuzingatia sheria zilizopo na iwapo sheria zitazingatiwa kila mmoja atampenda mwenzake na haki itatendeka kwani hakuna mtu yeyote au kiongozi yoyote atakaye mwonea mwingine.
“Sheria zipo na zinatakiwa kufuatwa na mwanzilishi wa sheria ni Mungu mwenyewe na sheria ya kwanza ya Mungu ni kuishi katika neno na utakatifu sambamba na agizo la watu kupendana.
“Kama watu wataishi kwa neno la Mungu na kutimiza sheria zake na kwa kupendana na kuaminiana ni wazi kuwa hakutakuwepo na watu ambao wanaitwa mafisadi au wapiga dili na watu watakuwa wamekomaa Kiroho”alisisitiza Mchungaji Siliti.
Akizungumzia baadhi ya wakristo ambao wamedumaa Kiroho ni kutokana na kutokuwa waaminifu katika kumtii Mungu na kutokufuata sheria ya Mungu alizoziweka na kutii na upendo.
Alisema kuwa wapo wakristo wengi ambao wanajiita walikole lakini hawaoneshi matendo yampasayo kuyafanya ya Kimungu badala yake wanafanya matendo maovu jambo ambalo linadhihilisha kuwa ni kutokuwa waaminifu katika kutii sheria za Kimungu.
“Lazima kufuata sheria za Kiroho ambazo zinatokana na nguvu ya Kimungu,kwani maandiko matakatifu yanaelekeza wazi kuwa amri mpya ambayo Mungu aliitoa ni kupendana kama alivyowapenda wanadamu“ameeleza Mchungaji Siliti