November 14, 2024

Mhe. Mwinjuma Abainisha Vipaombele Vya Wizara Kwa Mwaka 2023/24

0

 

Na Mwandishi Wetu,
Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Hamis Mwinjuma amesema kuwa moja ya  vipaumbele cha wizara kwa mwaka wa fedha 2022/24 ni kuimarisha miundombinu ya michezo  kwa kujenga Viwanja vipya viwili Jijini Dodoma na Arusha ikiwa ni muendelezo wa kujipanga  kuwa mwenyeji wa mashindano ya AFCON mwaka 2027 kwa kushirikiana na nchi za Kenya na Uganda.

Mhe. Mwinjuma ameyasema hayo Agosti 26 2023 Kibaha Pwani mbele ya Waheshimiwa Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala wa mikoa wakati akiwasilisha taarifa ya vipaumbele vya Wizara hiyo kwa mwaka  2023/2024 kwenye mafunzo ya kuwajengea uwezo viongozi hao.


 Amesema Serikali kwa kushirikiana na wadau imepanga kufanya ukarabati mkubwa wa uwanja wa Benjamin Mkapa pamoja na kuimarisha  miundombinu ya michezo katika shule maalumu 56 za Michezo pamoja na  ujenzi wa vituo vya mazoezi na kupumzikia wananchi na kwa kuanzia amesema ujenzi umeanzia katika mikoa ya Dodoma na Dar es salaam.

Naibu Waziri Mhe. Mwinjuma amebahinisha Vipaumbele vingine   kuwa, ni kuendelea kugawa mikopo kwa Wadau wa Utamaduni na Sanaa vingine ambapo hadi  kufikia Agosti 2023 Mfuko huo  umefanikiwa kutoa mikopo katika awamu mbili yenyec thamani ya shilingi Bilioni 1,077,000,000 kwa miradi 45 ya utamaduni na sanaa pamoja na kuendelea kugawa Mirabaha kwa kazi za  wabunifu na Waandishi wa fasihi.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

You cannot copy content of this page