Migodi yashauliwa kuwa sehemu ya kusaidia serikali suala la ajira.
SHIRIKA la kutetea Haki za Binadamu Kahama(SHIHABI) Mkoa wa Shinyanga limeishari migodi Midogo, ya kati na mikubwa kuwa sehemu ya kuisaidia serikali utoaji wa ajira nyingi kwa wananchi katika maeneo wanakowekeza.
Ushauri huo ulitolewa na mwanasheria wa shirika hilo Alex Makabe aliyeongozana na timu ya wajumbe wa shirika hilo kwenye ziala ya kutembelea mgodi huo kwa lengo la kujilidhisha kama Mgodi huo unazingatia masuala ya haki za binadamu na sheria za kazi.
Pia Mgodi huo umeombwa na shirika hilo kuzingatia suala la haki za binadamu kwa wafanyakazi wake ikiwemo suala la mikataba ya ajira, kuwaunganisha wafanyakazi na mifuko ya hifadhi ya jamii kama NSSF na mifuko mingine pamoja na kuzingatia suala la usalama kazini PPE.
Mwanasheria huyo akizungumza na waandishi wa Habari mara baada ya ziara hiyo alisema shirika linataka kuona kama migodi midogo midogo na ile ya kati uongozi unazingatia matakwa ya kisheria, wafanyakazi wake kuwa na mikataba ya ajira, wanapewa haki zao za msingi, mafao yao ya NSSF yanapelekwa na mwajiri?
Mwanasheria Makabe alidai kuwa shirika hilo limebaini mapungufu ya kiuongozi kwenye mgodi huo na kwamba mgodi huo hauna afisa rasilimali watu ambaye kimsingi ndiye anayejua suala la sheria ya haki za wafanyakazi wake na kuongeza kuwa kwenye mgodi huo meneja ndiye anayefanya kazi zote badala ya afisa rasilimali watu jambo ambalo siyo takwa la kisheria.
Pamoja na mambo mengine mwanasheria huyo wa SHIHABI alisema kuwa lengo kubwa la kuanza ziara ya kutembelea migodi kubwa ni lile la ajira za watoto chini ya miaka 18 suala la usalama kwa matumizi ya sumu kali aina ya ZEBAKI, SYANIDE kwenye mialo katika migodi midogo.
Aidha mwanasheria huyo ameshauri kuwa kunahaja ya mgodi huo kuwa na afisa rasilimali watu, mgodi huo kuwa wazi katika suala la mikataba ya wafanyakazi wake na kuongeza kuwa mapungufu mengine yaliyobainika ni kampuni kuajili wageni wengi kuliko watanzania.
“Kwenye suala la wafanyakazi kampuni imejitahidi kuajili lakini wageni ni wengi kuliko watanzania wachina wapo 11 na watanzania wapo 13 na kwamba hili halijakaa vizuri kisheria mimi nilitegemea kuona raia wa kigeni ni wachache na watanzania wanakuwa wengi na ili kuleta tija kampuni hiyo inapashwa kufanya marekebisho hapo kwani Tanzania wasomi ni wengi,Alisema mwanasheria Makabe.
Hata hivyo kwa upande wake Meneja wa Mgodi wa Sheng Long Mhandisi Bahati Buzuli alilipongeza shirika hilo la kutetea haki za binadamu (SHIHABI) kwa kufika katika mgodi wao na kubaini mapungufu hayo na kwamba lengo ni zuri na linaboresha ufanisi wa kazi kwenye kampuni yao.
Meneja huyo alitoa ahadi kwa waandishi wa habari katika mahojiano maalumu kuwa kwa ujio wa shirika hilo katika mgodi huo wa Sheng Long kampuni itatekeleza ushauri uliotolewa ili kuzidi kuboresha huku akikili kuwa kampuni haina afisa raslimali watu.
Alitumia fursa hiyo kueleza kuwa ajira nyingi wametoa kipaumbele kwa wananchi wazazwa wanaozunguka mgodi ili wanufaike na uwekezaji huo na kubainisha kuwa kuna miradi mingi watatekeleza kwenye jamii ya Msalala ikiwemo kuzingatia suala la CSR kwa kushirikiana na viongozi ngazi za vijiji na Halmashauri kwa ujumla.
“Tunampango wa kuhakikisha kuwa tunatengeneza ajira nyingi kwa wananchi hususani vijana na wanawake wawe sehemu ya kunufaika na uwekezaji kwenye nchi yao, mbali na mapungufu hayo tutaajili wataalamu wa kitanzania,” alisema Mhandisi Buzuli.
Shirika hilo limeanza ziara ya kutembelea migodi midogo, ya kati na mikubwa ili kujiridhisha na ajira kwa watoto wadogo chini ya miaka 18, suala la usalama kazini, stahiki kwa wafanyakazi pamoja na mikataba ya ajira likiwemo suala la matumizi ya zebaki CYANIDE kwenye mialo huko migodi midogo ya wa wachimbaji.