Milioni 565 Kukamilisha Mradi Wa Maji Singida
JUMLA ya sh.Milioni 565 zimetumika katika kukamilisha mradi wa maji katika kijiji cha malaja kata ya Nkalakala,tarafa ya Nduguti Wilaya ya Mkalama Mkoa wa Singida.Anaripoti Danson Kaijage,Mkalama.
Akitamburisha mradi huo leo tarehe 23 Septemba 2023 kwa kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru kitaifa Abdalla Shaib Kaim,Meneja wa Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira (Ruwasa) Mkalama mhandisi Christopher Sanguda amesema kuwa mradi huo utawanufaisha wananchi 6,611.
Mhandisi huyo amesema kuwa mradi huo utakapokuwa umekamilika utasaidia wakazi wa kijiji hicho kupata maji ambayo kwao ilikuwa ni sehemu ya tatizo katika eneo hilo.
Wakati huo Mkuu wa Wilaya ya Mkalama Mosse Machali amewataka wananchi wa eneo hili kuhakikisha wanatunza mazingira na miundombinu ya miradi ya maendeleo ili kuendelea kuwanufaisha.
Naye Meneja wa TARURA Wilaya ya Mkalama,Mhandisi Rahabu Thomasi amesema kuwa matengenezo ya barabara za Mwendo-Mng’anda-Mwanga kilometa 12.39 na Ishenga -Lambi Kilometa 4.12 utagharimu kiasi cha sh 314,986,600 zilizotokana na tozo mbalimbali kwa mwaka 2022/2023.
Amesema kuwa mradi huo wa ujenzi wa matengenezo ya barabara utasaidia wananchi kurahisisha usafiri hasa kipindi cha masika kwa kata za Nduguti,Nkalakala,Mwanga,Ilunda,Kinyangiri na Wilaya kwa ujumla.
Kwa ujumla wake Wilaya ya Mkalama imefanikiwa kuzindua miradi mbalimbali ya maendeleo ipatayo 6 yenye thamani ya sh.Bilioni 1.7 ambayo imezinduliwa na mbio za kwenge,kukaguliwa na kuwekewa kwa jiwe la msingi.