November 14, 2024

Moto Wateketeza Mabweni Shule Ya Mingas, Wanafunzi Wanusurika Kifo

0

 Na Paul Kayanda, Kahama

MOTO mkubwa uliozuka katika shule ya Msingi Mingas uliopo katika eneo
la Mayila, Mtaa wa Nyihogo katika Manispaa ya Kahama Mkoani Shinyanga,
umeteketeza mabweni yote ya shule hiyo huku wanafunzi wakinusurika
baada ya kuokolewa na jeshi la zima moto na uokoaji la Wilayani humo
pamoja na ushirikiano mkubwa wa makundi ya wananchi.

Licha ya wanafunzi kulazimika kulala katika madarasa ya shule hiyo kutokana na athari za moto huo, wananchi wamelipongeza Jeshi hilo  kwa kutambua wajibu wao na kuonesha juhudi kubwa na weledi katika utekelezaji wa zoezi la uokoaji, ikiwa ni pamoja na kufika eneo la tukio kwa wakati. 


Kwa mujibu wa mashuhuda wa ajali hiyo iliyotokea Septemba 5 majira ya
saa 12 kuelekea saa moja jioni, chanzo cha tukio hilo ni jenereta lililokuwa likitumika katika mabweni hayo.

Shuhuda wa kwanza kufika katika eneo hil, Kidahi Njige alisema kuwa

kama jirani wa karibu na shule hiyo aliona moshi ukifuka kwenye
mabweni na kuchukulia ni hali ya kawaida pengine wanafunzi wanafanya
usafi kwa kuchoma takataka lakini moshi ulizidi na kuamua kusogea
ndipo akabaini kuwa ni mabweni ya wanafunzi wanateketea ndipo
alipowaamuru jamaa aliokuwa nao na kufika kwenye eneo la tukio.

Alisema kuwa haraka sana waliita jeshi la zimamoto huku wao wakiomba
msaada kwa watu wengine ambao walifika na kuanza kuokoa watoto
waliokuwa ndani ya mabweni hayo pamoja na vyombo vya wanafunzi hao, ikiwemo
magodoro, masanduku pamoja na nguo zao.


“Kwa kweli tunawapongeza jeshi la zima moto na uokoaji kwa kuwahi

ingawa vitu vikateketea kutokana na sababu mbalimbali zilizokuwa nje ya uwezi wa wao,”  alisema Shuhuda huyo.

Mkuu wa Jeshi la Zima Moto na Uokoaji Wilaya ya Kahama,
Mkaguzi Eduard Selemani alisema kuwa moto huo ulikuwa mkubwa na
umeteketeza vitu vingi na kabla ya maji kuisha walipambana nao mpaka
ukazima.

“Katika zoezi la kukabiliana na moto hakuna kifo chochote kilichotokea tofauti na vifaa vya wanafunzi na shule hiyo kuteketezwa,,” alisema. 

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa mtaa wa Nyihogo, Said Mitimingi alikili
kutokea kwa ajali hiyo huku akiwaahidi wananchi kwamba uchunguzi unaendea kufanyika kubaini chanzo cha kuzuka kwa moto huo, na kusema huwa hakuna aliyejeruhiwa katika ajari hiyo huku akiwaomba wananchi wazidi kuwa na ushirikiano kama huo.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

You cannot copy content of this page