Mpwapwa waweka Mikakati Ya Afya Ya Uzazi Na Mtoto
Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma Bw. Ally Gugu amefungua kikao cha Kamati ya Ushauri ya Mradi ya uboreshaji wa huduma za afya ya uzazi na mtoto kwa Halmashauri ya Mpwapwa kilichofanyika leo tarehe 30 agosti 2023 katika ukumbi wa Hospitali ya Mpwapwa.
Akizungumza katika kikao hicho Gugu amesema ni vyema kuzingatia mikakati iliyopo ili miradi ambayo ipo katika Halmashauri inakamilika kwa wakati na kuleta manufaa kwa wananchi.
Naye Katibu Tawala Msaidizi, Afya, Lishe na Ustawi wa Jamii Mkoa wa Dodoma Dkt. Best Magoma amesema kikao hicho kina lengo la kuhakikisha miradi ya KOFIH inatekelezwa kwa wakati na kuweka mikakati ya ukamilishaji wake.
“KOFIH imeleta miradi ya afya na vifaa tiba kwa ajili ya wananchi wa wilaya ya Mpwapwa hivo pongezi kwa KOFIH na kuna baadhi ya hospitali zilizofadhiliwa zimeshaanza kutoa huduma za afya ambazo zimejengwa kwa fedha za KOFIH ambapo mwanzoni wananchi hao walikuwa wanafuata huduma hiyo mbali na hospitali ya Wilaya na kuweza kupata mafunzo kwa watumishi”.amesema Mosha.