November 15, 2024

Mwenyekiti Wa Halmashauri Ushetu Aagiza Utatuzi Wa Changamoto Kwa Wananchi

0

 NA PAUL KAYANDA, KAHAMA

MWENYEKITI wa Halmashauri ya Ushetu, Wilayani Kahama Mkoani Shinyanga Gagi Lala ameisisitiza Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo chini ya mkurugenzi wake Hadija  Mohamed  kuendelea kutatua changamoto zilizopo ili kutenda haki kwa wananchi.


Pia ameitaka ofisi hiyo kuzingatia ushauri wa baraza la Madiwani kuzingatia changamoto ya ukusanywaji hafifu wa mapato chini ya asilimia miamoja na kutopeleka fedha kwa asilimia mia moja kwenye miradi ya maendeleo pamoja huku akisema kuwa kwa kuwa wanaanza upya wakawe makini sasa.

Aidha mwenyekiti huyo amesema kuwa pia katika Halmashauri hiyo ipo changamoto ya wakulima wa tumbaku nakutumia kikao hicho kuiomba serikali ihakikishe inalipa wakulima hao kwani ni haki yao.


Vile vile mwenyekiti huyo ameiomba  serikali kupitia wizara ya kilimo, maliasili, Mifugo na Uvuvi kutatua changamoto ya wakulima wa zao la tumbaku Ushetu ili walipwe stahiki zao kwakuwa wanategemea kilimo hicho kuendeshea maisha yao.

Hata hivyo Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri hiyo Hadija Mohamed Kubonela amelihakikishia baraza hilo utekelezaji mzuri wa miradi ya maendeleo kwa wananchi.

Amesema kuwa miradi mingi ilikuwa imepangiwa bajeti katika mwaka wa fedha unaoendelea, lakini iwapo miradi hiyo ilikuwa haijapangiwa bajeti mana yake haitaweza kutekelezwa.


 

Mkurugenzi huyo amesema kuwa anawahakikishia wajumbe wa baraza hilo kama miradi hiyo ipo katika bajeti ijayo itatekelezwa lakini wajumbe wakumbuke kuwa kama halmashauri ya Ushetu kwa mwaka wa fedha uliopita hawakukusanya mapato kwa asilimia miamoja.

 

Hata hivyo kwa upande wake makamu mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Emmanuel Makashi baada ya kuchaguliwa na wajumbe hao ili awaongoze tena tena kwa mara kipindi kingine huku akisema hata mwaka ujao wafanye hivyo tena.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

You cannot copy content of this page