Mwenyekiti Wazazi Taifa awapa Majukumu CCM Kahama Kuhusu Sekondari ya Wigehe
Na Paul Kayanda, Kahama
MWENYEKITI wa Jumuia ya Wazazi (CCM) Taifa Fadhil Maganya ameonesha kukitishwa na kitendo shule ya sekondari ya wazazi Wigehe cha kuwa na wanafunzi kumi wa kidato cha tano na sita ikiwa na ukarabati unaofanywa na Mbia aliyeingia mkataba wa kuendesha shule hiyo.
Wanafunzi wanaosoma katika shule hiyo fakati za pcb ambao wa jumla ya wanne, pcm mwanafunzi mmoja, cbg wanafunzi wanne pamoja na Hgl Mwanafunzi mmoja ambao wanafanya jumla yao kuwa wanafunzi 10.
Hatua hiyo imekuja baada ya Mkuu wa Shule hiyo ya sekondari ya Wigehe inayomilikiwa na Jumuia hiyo ya wazazi Charles Festo kutoa taarifa mbele ya Mwenyekiti huyo wa jumuia ya wazazi Taifa na kusema changamoto ambazo zipo katika shule hiyo ambapo nayo ni mojawapo.
Alisema kuwa licha ya kuitangaza shule hiyo katika vyombo mbalimbali vya habari lakini upatikanaji wa wanafunzi umekuwa mdogo hali ambao hadi sasa badao wanahangaika ili kuona inarudi katika hli iliyokuwa nayo katika siku za awali.
Alisema kuwa mbali na kuwa na wanafunzi kumi katika shule hiyo pia kumekuwa na uhaba wa walimu kwani katika shule hiyo kunamjumla ya wafanyakazi tisa huku kati yao walimu wa sita tuu na wale watumishi wa kawaida wakiwa watatu.
Mkuu huyo wa Shule hiyo aliendelea kusema kuwa bado wanaendelea na ukarabati wa awali katika maeneo mbalimbali yanayozunguka shule hiyo kama vile eneo la maabara, Mabweni ya kulala wanafunzi pamoja na ofisi mbalimbali za kiutawala katika eneo hilo la shule.
‘Ukarabati katika shule hiyo umeanza tangu mwezi januari na tayari tumekarabati jumla ya madarasa matatu, huku maabara ikionekana kukamilika tunaahidi katika siku za usoni tutaweza kumaliza baadhi ya changamoto ambazo zipo katika shule hii ya Wigehe”, Alisema Mkuu wa Shule hiyo.
Kwa upande wake Mwenyrkiti huyo wa Jumuia ya Wazazi Taifa Fadhili Maganya alisema kuwa kumekuwa na tabia kwa sasa ya kutosimia mali zinazomilikiwa na jumia ya wazazi kama ipasavyo na kuongeza kuwa katika uongozi wa sasa atahakikisha mali zote zinasimamiwa.
Hata hivyo Mwenyekiti huyo alisema kuwa ukarabati uliofanywa na Mbia katika shule hiyo ambayeni Shirika lisilo la Kiserikali la Cherish Foundation hauridhishi na kuwataka uongozi wa jumia hiyo ya wazazi kuhakikisha kuwa kazi inafanyika katika shule hiyo kwa harakazaidi.
“Mali za jumiua ya wazazi nimebaini hazisimamiwi vizuri, na hata ukarabati ulifanywa katika maeneo mbalimbali ya majengo ya shule hii hauridhishi kwa hiyo niona bora ziku moja nifanya ziara nchi nzima kwa lengo la kuna na kukagua mali za jumuia ya Wazazi kwa ukaribu zaidi”, Aliongeza Mwenyekiti wa Jumia ya wazazi Taifa Fadhili Maganya.
Katika ziara yake hiyo ya siku mbili katika Wilaya ya Kahama Mwenyekiti huyo alikagua baadhi ya miradi ya jumuia hiyo ikiwa ni pamoja na kiwanja cha ekari 53 ambzo katika siku nza baadaye zinatarajiwa kujengwa Hospitali ya Rufaa pamoja na chuo cha tiba na mardi mwingine ni ule wa vibanda 15 vilivyo katika eneo la uwanja wa magufuli mjini kahama.