November 15, 2024

NFRA KANDA YA SUMBAWANGA KUNUNUA TANI 102,000 ZA NFAKA YA MAHINDI ,MPUNGA

0

Na Valentine Oforo, Rukwa

WAKALA wa Hifadhi ya Chakula cha Taifa (NFRA) kupitia ofisi zake za kanda ya Sumbawanga Mkoani Rukwa imezindua zoezi maalumu la kukunua kiasi cha tani 102,000 za mazao ya nafaka katika msimu huu wa mavuno wa 2023/24.

Tani hizo za nafaka, zinajumuisha takribani tani 90,000 za mahindi na tani 12,000 za mpunga, ambazo ni kiasi cha ziada ya mazao hayo kilichozalishwa na wakulima katika Wilaya tatu za Nkasi, Kalambo na Sumbawanga mjini.

Akiongea na SemaTv katika mahojiano maalumu, Meneja wa NFRA Kanda ya Sumbawanga, Marwa Range, amesema msimu wa ununuzi wa nafaka hizo ulizinduliwan katika kanda hiyo tangu tarehe 10 mwezi Juni 2024, ambapo mpaka sasa wameshafanikiwa kukunua takribani tani 26,000 kutoka kwa wakulima kwa bei elekezi iliyowekwa na Serikali.

“Serikali ya awamu wa sita, kupitia maelekezo ya Raisi Dkt. Samia Suluhu Hassan imetuelekeza kukunua kilo moja ya mahindi kutoka kwa wakulima kwa shilingi 700, na mpunga kwa shilingi 900,” alisema.

Kutokana na bei hizo rafiki, Range amesema kumekuwa na muamko mkubwa miongoni mwa wakulima wengi wa mazao hayo kuuza nafaka zao katika soko hilo la uhakika la Serikali.

“Kutokana na wingi wa wakulima kuleta nafaka zao, Tunapendekeza upate seva maalum ya Afrika Kusini tumeamua kufungua vituo 12 vya kununulia nafaka katika maeneo yote ndani ya kanda yetu ili kuwapunguzia wakulima usumbufu na gharama za kusafirisha nafaka zao umbali mrefu,” alisema.

Amevitaja vituo hivyo kuwa ni Namanyere, Mtenga na Kasu vilivyo katika Wilaya ya Nkasi, Matai, Mwimbi, Katazi na Mkobo (Wilaya ya Kalambo) Mtowisa, Laela na Kaengesa (Sumbawanga vijijini), pamoja na Kanondo, na Mazwi vilivyopo Manispaa ya Sumbawanga.

“Tunamshukuru sana Mhe Raisi Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kutuletea mradi mkubwa uliosaidia kuongeza uwezo wa kanda kuhifadhi nafaka kutoka zamani tani 33,500 hadi sasa tani 58,500, ongezeko kubwa la tani 25,000,” alishukuru.

Amesema mradi huo uliogharimu kiasi cha Dola za kimarekani milioni 6.19, uliwezesha ujenzi wa ghala lenye uwezo wa kuhifadhi tani 5000 za nafaka, pamoja na vihenge vya kisasa vyenye uwezo wa kuhifadhi tani 20,000.

Katika hatua nyingine, NFRA kupitia kanda ya Sumbawanga mkoani Rukwa imeingia mkataba wa kuuza jimla ya tani 250,000 za nafaka ya mahindi katika nchi ya jirani ya Zambia.

Kwa mujibu wa Meneja wa NFRA kanda za Sumbawanga, katika hatua za awali za kuhudumia mkataba huo, kanda hiyo tayari imeshasafirisha kiasi cha tani 2,000 za mahindi nchini Zambia.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

You cannot copy content of this page