November 15, 2024

R Shinyanga Awaagiza DED /DC Kahama Kutatua Migogoro ya Ardhi Zahanati

0

 Na Paul Kayanda, Kahama

MKUU wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mdeme amemwagiza mkuu wa Wilaya ya Kahama Mboni Muhita kuhakikisha kuwa anasimamia uuzwaji holela wa ardhi katika eneo la Mtaa wa Shunu Manispaa ya Kahama pamoja na kutatua kero zinazohusu migogoro hiyo.

 

Mkuu huyo wa Mkoa ametoa agizo hilo leo Septemba 20 kwenye mkutano wa hadhara alioitisha baada ya ziara yake ya kikazi Wilayani Kahama iliyolenga kukagua na kujionea miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa na halmashauri za tatu za Msalala, Ushet na Manispaa hiyo.

 


Mdeme akiwa katika mkutano wa hadhara alipokea malalamiko na kero mbalimbali zilizowasilishwa na wananchi wa Mtaa wa Shunu asilimia kubwa ya kero ni upande wa Idara ya ardhi pamoja na idara ya afya.

 

Kufuatia hali hiyo Mkuu wa Mkoa pia alimwagiza Mkurugenzi wa Manispaa ya Kahama kufanya umaliziaji katika mradi wa jengo la Zahanati ya Shunu ili ianze kutumika na wananchi wapate huduma ya matibabu na baadaye aanzishe ujenzi wa Kituo cha afya.

 

Aidha Mdeme amewataka watumishi kujiepusha na migogoro ya ardhi kwani kero nyingi zimeonekana ni migogoro ya ardhi.



 Awali Mathias Mlekwa mkazi wa Nyahanga amesema kuwa ofisi ya ardhi ilipokonya maeneo yao bila kuwashirikisha huku Felister Sala akisema kuwa ofisi ya ardhi pamoja na ofisi ya mwenyekiti wa Mtaa Shunu hawampi ushirikiano kuhusu eneo lake alilopokonywa na Idara hiyo.

 

Hata hivyo mwananchi mwingine aliyejitambulisha kwa jina la Shang’ai mkazi wa Nyahanga ameiomba Halmashauri ya Manispaa kupitia idara ya ardhi wafike kwenye maeneo ya shunu kutatua uuzwaji holela wa ardhi ili kupunguza malalamiko ya wananchi.

 


“Naomba hospitali ya manispaa iwekwe wazi kuwa huduma ya mama na mtoto siyo bure ile sera ya kwamba mtoto chini ya miaka mitano ama mama mjamzito ijulikane siyo bure maana wananachi wanalalamika kuombwa pesa kama hawana wanaumia,” amesema mwananchi huyo.


 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

You cannot copy content of this page