November 15, 2024

RC Serukamba Akabidhiwa Mwenge Toka Tabora

0

 Na Danson Kaijage,Singida.

MKUU wa Mkoa wa Singida Peter Serukamba amepokea rasm mwenge wa uhuru kutoka Mkoani Tabora na aliyekabidhi ni Mkuu wa Mkoa wa Tabora,Balozi Batlida Briani.

Rc TABORA Balozi Batilida Buriani (mwanamke) akimkabidhi Mwenge Rc wa  Singida Peter Serukamba.
Makabidhiano yamefanyika leo tarehe 22 Septemba 2023 katika Wilayani Iramba mkoani Singida.


Akipokea mwenge wa uhuru Peter Serukamba amesema kuwa lengo kubwa la kuupokea mwenge ni kufanya uchechemuzi wa miradi pamoja kuhamasisha upendo,amani na ushirikiano.


Serukamba akizungumza muda mfupi baada ya kupokea mwenge amesema kuwa utazindua miradi mbalimbali ikiwepo miradi ya sekta ya elimu,afya miradi ya utunzaji wa Mazingira.


Akizungumzia miradi amesema kuwa katika kipindi cha kuanzia Julai 2022 hadi Septemba  2023 miradi yenye thamani ya fedha kiasi cha sh.bilioni 223.9 imetekelezwa na inaendelea kutekelezwa kwa fedha kutoka Serikali Kuu,Serikali za Mitaa na wadau mbalimbali wa maendeleo.


Amebainisha miradi ambayo inatekelezwa katika Mkoa wa Singida na Wilaya zake ni pamoja na sekta ya Elimu,Afya,Utawala,Kilimo,Uwezeshaji wananchi kiuchumi,Barabara,Nishati na Maji.



Akizungumzia sekta ya Elimu amesema kuwa Jumla ya sh.Bilioni 34.08 zimetolewa kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya miundombinu ya elimu hususani ujenzi wa shule mpya za BOOST na shule mpya za sekondari kupitia mradi wa SEQUIP pamoja na utoaji wa elimu bila malipo kutoka shule ya msingi hadi kidato cha nne.


Kwanupande wa kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Taifa  Abdalla Shaib Kalm amesema kuwa lengo la kukagua miradi hiyo ni kuhakikisha miradi inayotekelezwa inaendana na thamani ya fedha.



Amesema serikali inayoongozwa na Rais Dk.Samia Suluhu Hasani,imekuwa ikipambana kutafuta fedha kwa kwa ajili ya maendeleo hivyo ni jukumu la watendaji kuhakikisha wanasimamia miradi kwa thamani ya fedha inayotakiwa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

You cannot copy content of this page