November 14, 2024

SHILINGI BILIONI 3 KUDHAMINI JEZI ZA TIMU ZA TAIFA; DKT. NDUMBARO ASHUHUDIA UTIAJI SAINI

0

 

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro amelipongeza Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kwa kuendelea kuwatumia wawekezaji wa ndani kutengeneza jezi za mpira wa miguu wa timu za Taifa.


Dkt. Ndumbaro ametoa pongezi hizo Septamba 11, 2023 Jijini Dar es Salaam mara baada ya kushuhudia utiaji saini wa Mkataba wa Udhamini wa Jezi za Timu za mpira wa miguu za Taifa kati ya TFF na Sandaland Fashion Wear Ltd wa thamani ya Shilingi Bilioni 3 kwa muda wa miaka 5.


“Naipongeza Sandaland kwa kushinda zabuni hii, natoa rai kwenu kuongeza juhudi mfike nje ya mipaka ya Tanzania kwa kupata zabuni za kutengeneza jezi za klabu na timu za Taifa, naamini mtafanya hivyo” amesema Dkt. Ndumbaro.


Ameipongeza TFF kwa kusaini mkataba huo ambao utakua unawapa fedha, na kusisitiza kuwa uongozi wa Rais Walles Karia umefanikisha Tanzania kufuzu AFCON mara 2, timu ya Wanawake chini ya Miaka 17 na timu ya watu wenye ulemavu Tembo Warriors zimefika robo Fainali ya kombe la Dunia, huku Timu ya Wasichana ya Shule ya Sekondari ya Fountain Gate ya Dodoma, kuibuka mabingwa wa mashindano ya soka ya shule za Afrika ya CAF.


Kwa upande wake Rais Karia amesema Mkataba huo utahusisha Timu zote za Taifa za Mpira wa Miguu, ikiwa ni utekekezaji wa maagizo ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kutaka wawekezaji wazawa kupewa nafasi zaidi nchini, ambapo amesema wataongeza wadhamini wengi katika maeneo mbalimbali kama ilivyo pia katika Ligi Kuu.



Naye Mkurugenzi wa Kampuni ya Sandaland Mhe. Yusuph Yenga amesema Kampuni hiyo ina uzoefu wa kutengeneza jezi hapa nchini ambapo tayari wana Mkataba timu ya Simba na kuahidi kuwa jezi hizo zitakuwa na ubora na viwango vya hali ya juu



Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

You cannot copy content of this page