TAMASHA LA MAASAI FESTIVAL LIMEZINDULIWA ARUSHA RC ATAKA AMANI MSHIKAMANO UMOJA KUENDELEA KUDUMISHWA
Na Ahmed Mahmoud
Mkuu wa Mkoa wa Arusha John Mongela amewataka viongozi wa kijamii na Machifu kuendelea kudumisha misingi ya Mila sanjari na kutunza Amani mshikamano na Umoja wa Watanzania.
Aidha filamu ya Royal Tour imeleta mafanikio makubwa katika kusukuma biashara na ustawi wa jamii kwa Watanzania Moja ya kabila lililobeba urithi huo Kwa muda mrefu Pamoja na changamoto za mabadiliko ya Mfumo wa maisha ni Wamaasai.
Yamesemwa hayo Kwa niaba yake na Katibu Tawala Msaidizi Mkoa wa Arusha David Lyamongi wakati wa ufunguzi wa Tamasha la Utamaduni wa Wamaasai (Maasai Festival)inalofanyika siku tatu kuanzia Tarehe 8-10 Jijini Arusha
Amesema Tamasha la Wamaasai ni nguzo muhimu ya kuendeleza mshikamano na Umoja sanjari na tamaduni zetu ikiwemo utalii wa Utamaduni nchini mwetu unaoenda sambamba na kuvutia wageni kuongeza siku za kuwepo nchini hivyo ni busara kwao kupitia Tamasha hilo kuliendeleza na kulienzi Kwani kabila Hilo ni Moja ya makabila yaliotunza Mila zao.
“Niwaombe viongozi wa Mila zetu kujenga misingi ya Maendeleo ya tamaduni zetu hususani ujenzi wa kuendeleza tamaduni hizo Ili kuendelea kuvutia utalii huu wa Utamaduni baada ya wageni kutembelea vivutio vyetu wapate muda wa kuendelea kuwepo nchini na hivyo kuongeza mapato“
Awali Laigwanan Mkuu wa kabila Hilo nchini Izack Eriksongo amesema kwamba Utamaduni huo ni sehemu ya kuendeleza mshikamano baina yao nchini na wamekuwa wakishiriki matamasha yao maeneo mbalimbali nchini Kwa lengo la kukuza na kudumisha Mila yao.
Amesema kwamba kabila hilo litaendelea kudumisha Umoja mshikamano na Serikali sanjari na kuhamasisha Maendeleo kupitia Mila zao hivyo wale wachache wenye changamoto zao sio lengo la kabila Hilo hivyo kuomba kuendeleza ushirikiano huo.
Nae Meneja wa Kanda ya Arusha wa Tigo Amesema kwamba Tigo wanatambua na hawawezi kubaki nyuma lazima tuwe sehemu ya kuchochea Hilo linalofanyika hapa kukuza Utamaduni na Utalii ndio maana tupo hapa kuwaletea na sisi huduma zetu ambazo zinaweza kusaidia katika kukuza Utamaduni wetu na Utalii Kwa kuwa ni chanzo Cha mapato ya nchi.
Amesema kwenye Tamasha hilo wamekuja na huduma mbalimbali katika Banda lao Kwa siku zote tatu Kwa ajili ya Kutoa huduma Kwa jamii ikiwemo majawabu ya changamoto za malipo kama lipa Kwa Tigo pesa Kwa kutumia lipa namba lakini pia huduma za data.
Amesema kwamba wataendelea kuunga Juhudi za Serikali yetu ya awamu ya Sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan kukuza Utalii wa Utamaduni sanjari na Utalii nchini Kwa kuendelea kudhamini Tamasha hilo na kwenye Tamasha hilo wamekuja na bidhaa kadhaa zipatikanazo kwenye kampuni hiyo.
Kwa Upande wake Mkurugenzi wa Tamasha la Maasai Festival Saitabau Nkemwa Amesema Tamasha hilo lilianzishwa Kwa lengo la kutangaza Utalii wa kiutamaduni ndio maana wameanza na Wamaasai Kwa Sababu ni kabila lililodumu kwenye Tamaduni zake hadi Leo sanjari na kuunga Juhudi za Mh.Rais Samia Suluhu Hassan baada ya filamu ya Royal Tour kufungua utalii nchini.
Amesema kupitia Tamasha hilo lengo kuu ni kutangaza nchi yetu Ili kuvutia wageni nchini Petu na wamejipanga kuendeleza Utamaduni wa kabila hilo ambao umedumu na kuwa nembo ya Utamaduni wa mwaafrika hivyo huo ndio mwanzo na wataendelea kukuza na kuendeleza Tamasha hilo kila mwaka