Mgeni Rasmi katika siku ya pili ya Tamasha la Pili la Utamaduni Kitaifa, Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana leo Agosti 26, 2023 alikagua mabanda ya maonesho ya Utamaduni na Sanaa pamoja na huduma mbalimbali kutoka Taasisi za Serikali, Fedha na Wadau wengine.
Mhe. Chana ameongozana na viongozi mbalimbali kutoka Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakiongozwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Elimu, Utamaduni na Michezo Mhe. Husna Sekiboko, viongozi wa mkoa wa Njombe wakiongozwa na Kaimu Mkuu wa Mkoa huo Mhe. Kissa Gwakisa Kasongwa, Wakuu wa Idara za Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo.
Tamasha hilo la Kitaifa linalofanyika mkoani Njombe linaongozwa na kaulimbiu inayosema Utamaduni ni Msingi wa maadili, tuulinde na kuuendeleza.