November 15, 2024

TUMIENI MATOKEO YA SENSA KWA MAENDELEO YA TAIFA -KAMATI

0

 KAMATI ya Kudumu ya Bajeti ya Baraza la Wawakilishi imesisitiza matumizi ya Takwimu kwani ni muhimu kwa maendeleo ya wananchi na Taifa kwa ujumla.


Aidha, imewapongeza Rais Dk.Samia Suluhu Hassan na Dk.Hussein Ally Mwinyi kwa kazi kubwa wanayofanya katika kuhakikisha wananchi wanapata Maendeleo.



Hayo yamebainishwa leo Julai 23, 2024 na Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mwanaasha Khamisi Juma, wakati wa ziara ya mafunzo kwa wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wa kamati hiyo pamoja na Watendaji kutoka Ofisi ya Rais Fedha na Mipango Zanzibar.


“Takwimu sahihi ni muhimu kwa Maendeleo ya wananchi na Taifa kwa ujumla hivyo ni muhimu kuendelea kuzitumia Kwa maslahi mapana ya Taifa,”amesema


Ameongeza kuwa:”Tunawapongeza viongozi wetu Wakuu Rais Dk.Samia na Dk. Hussein kwa maono yao na kazi kubwa wanazofanya Kwa maslahi ya wananchi.



Kwa upande wake Naibu Waziri Ofisi ya Rais Fedha na Mipango wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Juma Makungu Juma amesema takwimu ni muhimu kwa Maendeleo ya nchi.


Amesema ukosefu wa takwimu ni sawa na kwenda vitani bila siraha lazima utashindwa ndio maana viongozi wakuu wanasisitiza matumizi ya takwimu.


“Tunapoenda kuelimisha umuhimu watakwimu itasaidia kutoa elimu kwa wananchi. Kumekuwa na ushurikiano mzuri kati ya Ofisi ya takwimu ya Tanzania bara na Zanzibar Kwa maslahi ya Taifa,”amesema



Naye Mtakwimu Mkuu wa Serikali Dk.Albina Chuwa amesema ni maono ya Rais Dk Samia na Dk.Huseein Ally Mwinyi kwa kuendelea kutoa kipaumbele katika kuendeleza takwimu rasmi nchini.


“Sensa ya watu na makazi ya iliyofanyika mwaka 2022 imeleta heshima kwasababu ilifanyika kisasa na kwa ufasaha wa Hali ya juu kutokana na maona ya viongozi wetu.



Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

You cannot copy content of this page