November 14, 2024

Vijana Wa Dini Ya Kiislamu Wasisitiziwa Kulinda Amani Na Kufanyakazi Kwa Bidii

0

 Na Peter Mkwavila DODOMA

JUMUIYA ya vijana wa Kiislamu wilaya ya Dodoma (JUVIKIBA) wameshauriwa kuilinda na kudumisha amani ya Nchi kwa gharama yoyote,huku wakisisitizwa pia kufanya kazi kwa bidii ili kujiletea maendeleo yao ya  kiuchumi.

Vijana kutoka Jumuiya ya Juvikiba wilaya ya Dodoma wakishiriki kufanya usafi kwenye makaburi ya wahanga yaliyopo miyuji Jijini Dodoma kuelekea sikukuu ya Maulindi itakayofanyika septemba mwaka huu kitaifa Dodoma. 


Aidha wametakiwa pia kuhakikisha wanashiriki shughuli mbalimbali za kijamii na kidini badala ya kusubiri kushurutishwa na serikali pamoja na viongozi wa dini.

Ushauri huo umetolewa na Mwenyekiti wa Jumuiya ya vijana wilaya ya Dodoma Rashidi Ally alipokuwa akizungumza na vijana waliojitokeza kwenye zoezi la usafi wa mazingira uliofanyika katika makaburi ya wahanga yaliyopo kata ya Miyuji pamoja na Kizota Jiji la Dodoma.

Akizungumza kwenye zoezi hilo likiwa ni sehemu ya maandalizi ya  kuelekea sikukuu ya maulidi itakayofanyika kitaifa mwezi Septemba mwaka huu Dodoma ambaye Rais Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa mgeni rasm .

Mwenyekiti huyo amewataka vijana hao wa Kiislamu kuonyesha mfano kwa vitendo katika kuhakikisha amani iliyopo inalindwa kwa gharama yoyote huku wakishiriki kikamilifu katika kufanya shughuli za kijamii.

“Nina amani kwa mujibu wa dini yetu ya Kiislamu  kwa kufanya hivyo watakuwa wameyaenzi kwa mafunzo na matendo ya Mtume Muhammad (S.A.W) kama alivyokuwa akifanya kwa watu wake”alisema.

Pia kwa kufanya hivyo katika kushiriki shughuli za kijamii watakuwa wamemuunga mkono Mufti mkuu wa Tanzania shehe Dk Abbakar Zuber ambaye amekuwa akisisitiza waumini wa dini ya kiislamu kujitambua,kubadili na kuacha mazoea.

Naye Katibu wa Jumuiya hiyo ya vijana wilaya ya Dodoma Bashuru Mdoe amewakumbusha vijana wa dini ya kiislamu kuunda vikundi ili waweze kupatiwa mikopo ambayo itakayowawezesha kuanzisha miradi itakayowakwamua kiiuchumi badala ya kukaa na kulaumu serikali kwa kushindwa kuwajali.


Alisema kwa hivi sasa Dodoma kuna fursa mbalimbali zikiwemo za kidini na kiserikali wakiunga kwa pamoja wanaweza kupatiwa hiyo mikopo ambayo wanayoweza kuipta ndani ya Halmashauri zao pamoja na taasisi za kifedha zinazokubalika kwa upande wao.

“Niwahamasishe vijana wezangu Serikali ina fursa nyingi kwa ajili ya makundi ya vijana hivyo unganeni kwenye vikundi ili muweze kupata mikopo hiyo kutoka kwenye taasisi zinazokubalika kwa upande wao na kwenye Halmashauri”alisema

Mratibu wa Jumuiya hiyo ya kidini ya Kiislamu mkoa wa Dodoma Omary Nguzo amewahimiza vijana kusoma elimu ya dini ili waweze kuepukana na mafundisho ya mmomonoko wa maadili mabovu ambayotolewa kupitia kwenye mitandao.

Alisema wao wakijikita kwenye kusoma elimu ya kidini wataweza kuisaidia serikali kwa kupinga mitandayo ambayo imekuwa ikipotosha vijana wengi na kujikuta wakiinga matendo yasiyo na maadili kwa nchi yatu.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

You cannot copy content of this page