Alisema kuwa badala ya kusubiri serikali itoe ajira kwa upande wao wanatakiwa kujikita kwenye kilimo,uvuvi na ufugaji ambapo utawawezesha kujiajiri wenyewe na kuajiri vijana wezao.
“Wilaya yetu ya Bahi ina sifa ya kuwepo kwa sekta mbalimbali ambazo zinazoweza kuwabadilisha vijana kimaendeleo na kiuchumi,hivyo niwaomba badala ya kusibiri ajira kutoka serikalini ni vema wakajikita kwenye fursa hizo ambazo zitawabadilisha maisha yao”alisema.
Sangulah pia amewataka vijana wa wilaya hiyo kuiunga mkono serikali kwa juhudi zinazofanywa katika kuliletea Taifa maendeleo yake,huku pia wakikataa kutumiwa na watu wasioitakia mema nchi hii kwa lengo la kuharibu amani.
Awali akifungua kikao cha baraza hilo la vijana Mbunge wa jimbo la Bahi Kenneth Nollo amewataka kuungana kwa pamoja ili waweze kuanzisha vikundi vitakavyowawezesha kupata mikopo itakayowawesha kupata miradi mbalimbali.
Alisema kuwa serikali chani ya utawala wa Chama cha mapinduzi kiko tayari kuwasimamia kwenye vikundi ambavyo vitakavyo anzishwa kwa ajili ya kuhakikisha mnapata hiyo mikopo ambayo kwa upande wenu itawabadilisha mitizamo ya maisha yenu.
Pia amewataka vijana hao wa wilaya ya Bahi kuhakikisha wanajiendeleza kielimu zaidi kupitia nafasi walizonazo ili waweze kuwasimamia wezao katika sekta mbalimbali zikiwemo za kijamii kiserikali kiroho na kichama kwa ujumla.
“Kwa kupitia kikao hiki cha baraza la vijana kikao hiki nafahamu kuwa naongea na nyinyi vijana ambao baadhi yenu ni viongozi,niwaombe basi mjiiendeleza kielimu zaidi ili muweze kuongoza wezenu na jamii inayowazunguka kisomi zaidi”alisisitiza.
Aidha Mbunge huyo amewaangiza vijana wa wilaya hiyo kuwa mabalozi wa kuwashawishi wezao kufanya kazi zinazokubalika ikiwemo za kilimo,uvuvi na ufugaji ambazo naamini zitawabadilisha maisha yao kiuchumi zaidi.