November 15, 2024

Wananchi Wapewa Rai Kushiriki Wiki Ya Kitaifa Ya Ufuatiliaji Na Tathmini

0

 Na; Mwandishi Wetu,  Dodoma


WANANCHI wametakiwa kushiriki katika Kongamano la kitaifa la ufuatiliaji na tathmini itakayofanyika Jijini Arusha kwa wiki moja mfululizo, ambalo litajikita katika utoaji wa elimu juu ya ufuatiliaji wa miradi mbalimbali ya kimaendeleo inayofanywa na Serikali katika maeneo yao.


Wito huo umetolewa leo ( 28 Agosti 2023) Jijini Dodoma na Mtakwimu Mkuu, Idara ya Ufuatliaji na Tathmini, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Bw. Thomas Saguda.

Bwn. Saguda amesema wananchi wanaweza kushirki na kujifunza mambo mbalimbali kupitia maonyesho yanayotarajiwa kufanyika katika Kongamano hilo muhimu.

“Maonesho haya yatawapa fursa wananchi kujifunza namna wanavyopaswa kufanya ufuatiliajia na tathmini wa miradi mbalimbali inayotekelezwa na Serikali katika maeneo yao,” alieleza. 

Pamoja na hayo, ameongeza kuwa Kongamano hilo pia litahusisha mafunzo ya kitaaluma, warsha mbalimbali zitakazoendeshwa na wataalamu wabobezi wa masuala ya ufuatiliajia na tathmini kutoka ndani na nje ya nchi.

Aidha, kwa upande wake, Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Ufuatiliaji na Tathmini kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Bw. JohnBosco Quman, alisema eneo la ufuatiliaji  na tathmini linamgusa kila mwananchi.

Alifafanua kuwa, Idara hiyo ina jumuku kubwa la kuhakikisha kuwa miradi mbalimbali inayotekelezwa na Serikali inawanufaisha  jamii nzima katika maeneo husika.

Kongamano hili la Pili la Kitaifa la Wiki ya Ufuatiliaji na Tathmini litakalofanyika Jijini Arusha mapema mwezi Septemba, linawalenga wataalam wa Ufuatiliaji na Tathmini, Maafisa na Mameneja wa Miradi kutoka katika Taasisi zote za Umma, Taasisi Binafsi, makampuni, Asasi za Kiraia na mashirika ya Kimataifa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

You cannot copy content of this page