November 15, 2024

Wapenzi wamekutwa wamefariki Chumbani kwao Dodoma

0

 

WATU wawili wanaodaiwa kuwa ni wapenzi wamekutwa wamefariki dunia ndani ya chumba chao walichokuwa wamepanga katika eneo la Osterbay Kata ya Makulu jijini Dodoma kwa kili kinadaiwa kuwa ni wivu wa kimapenzi.

 


 

Miili ya watu hao ilikutwa ikiwa na majera ya kukatwa na kitu chenye ncha kali shingoni kwa wa mwanamke na tumboni kwa mwanaume.

 

Tukio hilo litokea majira ya saa nane ya usiku wa kuamkia jana, baada ya mwenye nyumba Donald Nembele, kusikia kelele za wapangaji wa nyumba yake ndipo akaenda kubomoa mlango na kukuta chumba kimejaa damu huku mwanaume akiwa anagalagala chini utumbo ukiwa nje.

 

Akizungumza tukio hilo Balozi wa mtaa huo Isaya Mabiliji alisema tukio hilo la mauaji katika mtaa wake ni la kwanza kutokeo katika eneo hilo na limewashtua watu wengi wa mtaa huo.

 

Alisema alikwenda katika eneo hilo baada ya kuitwa na mwenye nyumba hiyo, na baada ya kufika eneo la tukio alikuta tayari wawili hao wamefariki dunia kutokana na majeraha ambayo walikuwa nayo yaliyosababisha kupoteza kiasi kingi cha damu.

 

Alisema hadi sasa hakuna anayefahamu chanzo cha tukio hilo ambalo limechukua uhai wa wawili hao.

“tulipofika tumeukuta mwili wa mwanamke umekatwa shingoni na mwanaume amekutwa amechanwa tumboni huku utumbo ukiwa nje”alisema Balozi huyo

 

Alisema walipofika eneo la tukio walikuta mlango umefungwa na kulazimika kubomoa ndio wakakutana na miili ya wawili hao ikiwa imelowa damu.

 

“Kwa kweli inasikitisha sana kuona mauaji kama hayo yanatokea mtaani hapa huku wawili hao ambao inasadikiwa ni mume na mke wakiwa wamejifungia ndani,”alisema Mabiliji.

 

“Tukio kama hili sio zuri kabisa machoni mwa watu,hivyo jamii tusijichukulie hovyo hatua za kisheria na kusababisha vifo,”alisema Mabiliji.

 

Alisema kutokana na hali hiyo walilazimika kutoa taarifa polisi walitoa taarifa katika kituo cha Polisi,ndipo askari wakaja na kuichumua miili hiyo na taratibu nyingine za uchunguzi kuendelea.

 

Naye mwenye nyumba lilipotokea tukio hilo Donald Nembele, alisema ilikuwa majira ya saa nane usiku wakati akienda msalani kujisaidia.

 

Alisema wakati akienda msalani alisikia kelele katika chumba hiko cha wapangaji ndipo akaenda kubomoa mlango na kukuta mwanaume anagalagala chini kwenye damu huku mwanamke naye akiwa kwenye damu hizo zilizotapakaa kwenye chumba hiko.

 

Alisema baada ya kuona hivyo alikwenda kutoa taarifa kwa Balozi wa mtaa ndipo Balozi kwa kushirikiana na majirani wakaenda kutoa taarifa katika kituo cha polisi Chimwaga.

 

Mwenyekiti wa mtaa wa Msangalale Mgharibi ambako tukio hilo limetokea Leonard Ndama, alithibitisha kutokea kwa tukio hilo huku akidai kuwa hakuna taarifa rasmi za chanzo cha vifo vya wawili hao.

 

“Hili tukio kweli limetokea usiku wa kuamakia leo (jana) na hawa marehemu inasaidia kiwa kywa walikuwa wapenzi kwa muda sasa lakini jana ndiyo likatokea tukio hilo la maauaji”alisema

 

Alisema hivi sasa wanasubiri taarifa za uchunguzi kutoka polisi na kuhusu miili ya marehemu hao imepelekwa katika chumba cha kuhifadhia maaiti katika hospitali ya Rufaani mkoa wa Dodoma.

 

“Wawili hao hawakuwa wenyeji wa eneo hili mwanaume alikuwa anafanya shughuli za ujenzi lakini mwanamke inasemekana ni mwenyeji wa Shinyanga”alisema

 

 

Hata hivyo Nipashe ilimtafuta Kamanda wa Polisi mkoani Dodoma Martine Otieno ili kuthibitisha kutokea kwa tukio lakini hakuweza kupokea simu yake.

 

Kamanda wa polisi mkoa wa wa Dodoma Martin Otieno, alikili kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa chanazo ni wivu wa kimapenzi.

 

“Kweli tukio hilo limetokea majira ya saa 8 kwenda saa 9 usiku katika eneo hilo la Ostabay ambapo mwanaume aliyefahamika kwa jina moja na Amosi alimuua mpenzi wa Samira Mathias kwa kumchoma na kisu shingoni hadi kukata kolomeo lake.

 

“Lakini baadaye mwanaume huyo na yeye alijichoma kisu cha tumbo hadi utumbo kutoka nje na majirani walipovunja mlango walikuta analalamika walipokwenda kutoa taarifa polisi  na mwanaume naye walipokorudi walikuta amekufa”alisema Kamanda Otieno

 

Alisema jeshi la polisi mkoa wa Dodoma linaendelea na uchunguzi wa tukio ambalo limesababishwa vifo vya wawili hao.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

You cannot copy content of this page