WAUZAJI WA DAWA ZA KULEVYA WANYOOSHEWA KIDOLE
A DANSON KAIJAGE,DODOMA
MWANGALIZI wa Kanisa la Tanzania Assembles of God (TAG) Singida na Mkurugenzi wa Uinjilist Jimbo la Singida Kaskazini ,Rev Jakson Mgelwa Kiula amekemea vikali baadhi ya watu wanaofanya biashara ya dawa za kulevya na kueleza kuwa huo ni mpango wa kuangamiza mguvukazi ya vijana wa kitanzania.
Ametoa onyo hilo jana alipokuwa akihubiri katika mkutano mkubwa wa injili uliofanyika Ihumwa Jijini Dodoma chini ya mchungaji mwenyeji wa kanisa la TAG RCC Ihumwa Dodoma,Lameck Siliti.
Katika mahubiri hayo Kiongozi huyo wa Kiroho anekemea baadhi ya watu ambao wameachana na kazi harari na kujikita katika uuzaji wa madawa ya kulevya ambayo yanachangia kwa kiasi kikubwa kudhoofisha nguvu kazi ya vijana wa kitanzania.
“Kuna watu ambao tayari wameisha haribikiwa na akili wao wanajikita katika kuuza madawa ya kulevya na wanawauzia vijana wetu na kusabaisha vijana hao kupoteza mwelekeo jambo ambalo linasababisha kupotea kwa nguvu kazi ya vijana na kulifanya taifa kukosa wazalishaji.
“Nakemea kwa nguvu zote watu wanaojihusisha na biashara ya madawa ya kulevya achana na kazi hizo tafuta kazi nyingine za kufanya acha kabisa kuliangamiza taifa kwa kufanya biashara haramu”amesisitiza Rev Kiula.
Hata hivyo alisema kuwa kanisa na yeye binasfi anaungana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Samia Suluhu Hassani kwa kuhakikisha watoto wanalindwa na kupewa maadili bora ambayo yataendelea kulifanya taifa la Tanzania kuwa na misingi imara.
“Kana watoto hawatalindwa na kupewa malezi yenye maadili mazuri ni wazi tutakuwa na kizazi cha ovyo,lakini kama watoto watapewa misingi bora na kujengewa misingi yenye kumcha Mungu tutabaki kuwa na taifa lenye watu safi na uzalishaji utaongezeka kwa kiwango cha juu”alisema Rev Kiula.
Katika hatua nyingine amewaonya viongozi mbalimbali wa Kiserikali na Kiimani wametakiwa kutokubali kuingia katika makubaliano ya ovyo na mataifa ya nje ambayo yanaweza kusababisha machafuko kwa kurubuniwa kwa kupewa misaasa au kutishiwa kunyimwa misaada pale ambapo watakakaa kuingia katika makubaliano yenye nia ovu kwa taifa.
Rev Kiula alisema kuwa kitendo cha kiongozi yoyote kuingia kwenye makubaliano ambayo ni ya ovyo na halengi kuwanufaisha watu husika na badala yake yanalenga kuligawa taifa au kuchochea vitendo viovu ambavyo havifai kitendo hicho moja kwa moja kinaonesha wazi kuwa aliyefanya makubaliano hayo ameharibikiwa na akili.
Alisema kuwa ni bora kuishi maisha ya kawaida na kufanya kazi kwa mikono yao kuliko kuingia katika makubaliano ya ovyo kwa kuofia kunyimwa misaada na mataifa makubwa au kupewa misaada kwa mashariti ambayo ni magumu na hayana faida kwa taifa.
Alisema kuwa kwa sasa yapo mataifa ambayo viongozi wake tayari wameisha haribikiwa hakili na wamekuwa wakishawishi baadhi ya nchi kuingia kwenye ndoa za jinsia moja kwa kueleza kuwa wakifanya hivyo watapatiwa misaada mbalimbali ya kimaendeleo bila kujua kuwa huo ni uasi mbele za Mungu na kwa kuwaza huko ni dalili za kuharibikiwa na akili.