November 14, 2024

Wazazi Watakiwa Kuwalinda Watoto Dhidi Ya Wimbi La Mmomonyoko Wa Maadili

0

 Na Paul Mabeja, Dodoma 


KUTOKANA na kukithiri kwa vitendo vya mmomonyoko wa maadili nchini, wazazi wametakiwa kuwalinda watoto wao ili wasiharibiwe na tamaduni za kigeni ikiwemo kujihusisha na vitendo vya ndoa za jinsia moja.

Rai hiyo imetolewa na Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Dodoma, Pilly Mbaga, kwenye mahafali ya kwanza ya darasa la saba katika Shule ya Awali na Msingi ya East Africa ya Jijini Dodoma. 

Mbaga ametahadharisha kuwa kwa sasa Dunia imeharibika sana hivyo wazazi wanao wajibu wa kuhakikisha wanawalinda watoto wao ili wasiharibiwe na tamaduni za mataifa mengine.


“Hivi sasa ndugu zangu dunia imeharibika sana vitendo vya mmomonyoko wa maadili vimekithiri sana hivyo wazazi mnapaswa kuwalinda watoto ili wasiharibiwe na tamaduni za mataifa mengi.

“Mataifa ambayo yamekuwa yakihamasisha masuala ya ndoa za jinsia moja na mambo mengine ambayo ni kunyume ya tamaduni za kitanzania na nikinyume na mpango wa Mungu” alisema.

Aidha, amewataka wazazi kuacha tabia ya kutelekeza suala la malezi ya watoto kwa walimu pekee yao bali wanapaswa kuwasimamia na kuwafuatilia kila wakati ili wabaini vikwazo ambayo wanakabiliwa navyo.

“Wazazi hatupaswi kuacha suala la malezi kwa walimu pekee yao bali tuhakikishe kuwa tunawafuatilia watoto wetu kwa kushirikiana na walimu ili kuwasaidia wasiingie kwenye mikono ya shetani hali ibadilika sana hivi sasa watoto wamekuwa na tabia za ajabu ambazo kama hatutakuwa makini nao tutawapoteza” alisema.


Kadhalika, amewataka walimu kuhakikisha kuwa wanasimamia watoto hasa wanapokuwa katika mabweni ili kubaini kama kuna mabadiliko yoyote ya kitabia na kuchukua hatua mapema kabla ya kundi kubwa kuharibiwa.

Vile vile, ameipongeza shule hiyo kwa kuunga mkono wa jitihada za serika katika uwekezaji kwenye sekta ya elimu ili kutoa elimu bora kwa watoto wa Kitanzania.

“Mkurugenzi niwapongeze sana kwa uwekezaji huu katika sekta ya elimu sisi chama pamoja na serikali kwa ujumla tutaendelea kutoa ushirikinao kwenu ili mfikie malengo yenu”alisema

Alisema azma ya serikali ya awamu ya sita ni kuboresha elimu ambapo hivi sasa imefanya uwekezaji mkubwa katika ujenzi wa madarasa,maabara, mabweni pamoja na miundombinu mingine ili kuinua kiwango cha elimu nchini.

Awali Mkurunzi wa shule hiyo Dk. Rose Rwakatare, ameishukuru serikali kwa kuendelea kuweka mazingira rafiki kwa wawekezaji wazawa.

“Serikali ilipohamia hapa wakati wa hayati Rais Magufuli alitoa wito kwa wawekezaji kuwekeza miundombinu mbalimbali ili kusaidia kutoa elimu na sisi kama watua mabo tumebobea katika elimu tuliamua kuwekeza kwa kujenga shule hii ili kuweza kutoa elimu bora”alisema

Hata hivyo, alisema lengo la shule hiyo ni kuunga mkono jitihada za serikali katika utoaji wa elimu bora kwa watoto wa kitanzania ili kuwawezesha kutoa ushindani katika soko la ajira duniani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

You cannot copy content of this page