WAZIRI CHANA ATETA NA BALOZI CHEN
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Balozi, Dkt.Pindi Chana (Mb) amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa China nchini Tanzania, Mhe. Chen Mingjian kuhusu kushirikiana katika maeneo mbalimbali ya Sekta ya Maliasili na Utalii hususan kuwekeza kwenye maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya uwekezaji.
Kikao hicho kimefanyika leo Oktoba 9, 2024 Mkoani Njombe katika hoteli ya Hillside.
Akizungumza katika kikao hicho, Mhe
Chana amehimiza wawekezaji kutoka nchini China kuwekeza hasa katika maeneo ambayo hayajaendelezwa ya Kusini mwa Tanzania.
Kwa upande wake Balozi Chen pamoja na mambo mengine amesema China iko tayari kushirikiana na Tanzania katika kuwekeza kwenye Sekta ya Utalii na kufafanua kuwa kwa sasa China inatekeleza Mradi wa Ngorongoro Lengai Geopark katika Hifadhi ya Ngorongoro.
Balozi Chen yuko Mkoani Njombe kwa ziara ya kikazi ambapo atazindua Kliniki ya Madaktari Bingwa kutoka nchini China, kutembelea kiwanda cha Nondo kinachomilikiwa na Wachina pamoja na kuzungumza na Wafanyabiashara kutoka nchini China.