Waziri Jafo Aipa Kongole STAMICO Kwa Utunzajia Mazingira
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo
ametoa pongezi kwa Shirika la Madini la Taifa STAMICO kwa kuunga mkono juhudi
za Serikali za kuhifadhi mazingira.
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo
akizungumza wakati wa zoezi la upandaji miti mkoani katika Viwanja vya
Bombambili (EPZA) mkoani Geita ambako yanafanyika Maonesho ya Kimataifa ya
Teknolojia ya Madini leo Septemba 25, 2023.
Ametoa
pongezi hizo aliposhiriki zoezi la upandaji miti mkoani katika viwanja vya
Bombambili (EPZA) mkoani Geita ambapo amewshukuru kwa kutekeleza maagizo aliyoyatoa
Agosti 12, 2022 wakati wa Maadhimisho ya Miaka 50 tangu kuanzishwa kwa STAMICO.
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo
akipanda mti katika Viwanja vya Bombambili (EPZA) mkoani Geita ambako
yanafanyika Maonesho ya Kimataifa ya Teknolojia ya Madini leo Septemba 25,
2023.
Amesema
kuwa shirika hilo lilikuja na Kampeni ya STAMICO na Mazingira at 50! kwa lengo
la kuhakikisha pamoja na uendeshaji wa shughuli za uchimbaji wa madini
kuhakikisha mazingira yanatunzwa kikamilifu.
“Mtakumbuka
nilifanya ziara ya kushtukiza kutembelea eneo la Ipagala (Dodoma) kuona kama
kweli mmetekeleza kwa vitendo maelekezo, nimekuta kweli mmetekeleza yote kwani
niliona mmezungushia uzio na miti inaendelea vizuri sana,” amesema Dkt. Jafo.
Waziri wa Madini Mhe. Anthony Mavunde akipanda mti katika Viwanja vya Bombambili (EPZA) mkoani Geita ambako yanafanyika Maonesho ya Kimataifa ya Teknolojia ya Madini leo Septemba 25, 2023.
Pia,
ameshukuru STAMICO kwa kufanya kazi kwa pamoja na vikundi mbalimbali vikiwemo Kikundi
cha Wanawake na Samia ambapo walipewa kazi ya kazi ya kupanda na kutunza miti 560
eneo la EPZA ambayo inazidi kustawi.
amewasifu kwa kuwapa uwakala ya kuuza nishati mbadala ya kupikia kwa Mkoa wa
Geita, hatua itakayosaidia katika kuhifadhi mazingira kuepouka ukataji wa miti
ovyo.
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo
akiwanawisha viongozi na wadau mara baada ya kushiriki katika zoezi la panda
mti katika Viwanja vya Bombambili (EPZA) mkoani Geita ambako yanafanyika
Maonesho ya Kimataifa ya Teknolojia ya Madini leo Septemba 25, 2023.
Katika
zoezi hilo jumla ya miti 340 ilipandwa pia na viongozi wengine akiwemo Waziri
wa Madini Mhe. Antony Mavunde, Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Geita ambaye pia ni Mkuu
wa Wilaya ya Nyang’wale Grace Kingalame
pamoja na viongozi wengine.